Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Mapigano makali yazuka tena mashariki Kongo DRC



Mapigano makali yazuka tena mashariki Kongo DRC
Mapigano makali yameripotiwa kutokea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23. Maafisa wa jeshi la Kongo wameripotiwa na duru za habari wakisema kuwa, mapigano hayo yametokea kati ya pande mbili katika jimbo la Kivu Kaskazini. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi zilizoripotiwa kuhusiana na matokeo ya mapigano
hayo. Wiki iliyopita Jean-Marie Runiga kiongozi  mwandamizi wa kundi la waasi wa M23 alionya kwamba, harakati hiyo inapanga kuanzisha mashambulio hivi karibuni dhidi ya vikosi vya serikali endapo serikali ya Kinshasa itakataa kufanya mazungumzo na kundi hilo. Kwa miezi kadhaa iliyopita kiongozi wa waasi hao wa Kongo amekuwa akiishi Kampala mji mkuu wa Uganda ambako amesema anazungumza na Rais Yoweri Museven ili kujaribu kuanza mazungumzo na serikali ya Kinshasa.

No comments:

Post a Comment