Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 29, 2012

Utawala wa Saudia waharibu athari za Kiislamu Madina



Utawala wa Saudia waharibu athari za Kiislamu MadinaUtawala wa Saudi Arabia unaendelea kuharibu turathi za Kiislamu zilizokuwa zimebakia katika mji wa kihistoaria wa Madina.
Kwa mujibu wa gazeti la Uingereza la Independent, katika miezi ya hivi karibuni Wasaudia walibomoa athari nyingi za Kiislamu zilizokuwa zimebakia katika maeneo tofauti ya mji mtakatifu wa Madina kwa kisingizio cha ukarabati wa nyumba zilizochakaa katika mji huo. Katika ripoti hiyo imeelezwa kuwa, utawala huo wa Aal Saud umebomoa misikiti mitatu inayohesabika kuwa ya kihistoria katika
ulimwengu wa Kiislamu na kwamba, hapo baadaye pia utawala huo unatazamiwa kubomoa msikiti mwingine wa kihistoria kwa kisingizio cha kujenga msikiti mkubwa mjini hapo. Aidha utawala wa Aal Saudi unatazamiwa kuanza oparesheni za kubomoa msikiti wa Mtume Muhammad (SAW) kuanzia mwishoni mwa mwezi ujao na sambamba na kumalizika kwa msimu huu wa hija. Eneo kubwa litakalokumbwa na oparesheni hizo ni lile la magharibi mwa msikiti huo wa Mtume (SAW) ambalo ndiko kuliko na haram ya mtukufu huyo.

No comments:

Post a Comment