Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, October 15, 2012

Wapinzani Kongo wataka kukomeshwa mapigano



Wapinzani Kongo wataka kukomeshwa mapigano Wapinzani nchini Kongo wametaka kukomeshwa vita huko mashariki mwa nchi hiyo kufuatia kuendelea mapigano katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.  Lucien Mbusa Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Kongo amesisitiza kwamba wapinzani nchini Kongo wanataraji kuwa Ufaransa itatumia ushawishi ilionao katika taasisi za kimataifa na hivyo kufanya juhudi za kumaliza mapigano mashariki mwa nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Lucien Mbusa ambaye ni mjumbe wa wapinzani katika bunge la Kongo
amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Francois Hollande wa Ufaransa mwishoni mwa kikao cha Francophone mjini Kinshasa.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi wa Kongo amesifu matamshi ya Rais wa Ufaransa  kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo ni yenye kutia shaka,  kwamba kuna ukiukaji wa haki za binadamu na pia raia wa Kongo wanafungwa jela bila ya kuhukumiwa.

No comments:

Post a Comment