Nour al Maliki amesema hayo katika safari yake nchini Russia na kuituhumu Ankara kwamba inajaribu kuiingiza NATO katika mgogoro wa Syria na kwamba shirika hilo la kijeshi la Magharibi halipaswi kuingilia mgogoro huo kwa kisingizio cha kuitetea Uturuki.
Waziri Mkuu wa Iraq pia imekosoa misimamo ya Ankara kuhusiana na mgogoro wa Syria na kusema kwamba, mtu anaweza kufikiri kuwa Uturuki inafanya kana kwamba ndio yenye jukumu la kutatua mgogoro huo kuliko hata wananchi wa Syria wenyewe. Maliki ametoa matamshi hayo akimjibu Katibu Mkuu wa NATO Andres Fogh Rasmussen aliyedai kuwa, shirika hilo la kijeshi la Magharibi linajitayarisha kuisaidia Uturuki dhidi ya Syria.
No comments:
Post a Comment