Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, October 18, 2012

Sheikh Dor akamatwa Kenya kuhusu MRC

Sheikh Dor akamatwa Kenya kuhusu MRC
Mbunge wa viti maalumu nchini Kenya Sheikh Mohammad Dor ametiwa mbaroni mjini Nairobi kufuatia matamshi yake ya wiki iliyopita aliposema kama angalikuwa na uwezo  angefadhili kundi la Mombasa Republican Council MRC.
Sheikh Dor ametiwa mbaroni siku chache baada ya polisi kuanzisha msako wa watu wanaounga mkono kundi la MRC katika eneo la Pwani ya Kenya. Kundi la MRC linataka eneo la pwani lijitenge na Kenya.
Katibu wa kudumu katika Wizara ya Usalama nchini Kenya, Mutea Iringo amesema kwamba, msako huo utaendelea hadi hali ya kawaida irejee katika eneo hilo.
Polisi nchini Kenya imesema kuwa, wanasiasa na wafanyabiashara wanaofadhili kundi la MRC watatiwa mbaroni na kufunguliwa mashtaka.
Hivi karibuni polisi walimtia mbaroni kiongozi wa MRC Omar Hamisi Mwamnwadzi pamoja na makumi ya wafuasi wa kundi hilo.

No comments:

Post a Comment