skip to main |
skip to sidebar
kusimama kidete ndiyo siri ya ushindi dhidi ya adui
Kamanda Mkuu wa Jeshi Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran
(SEPAH) amesema kuwa, kusimama kidete wananchi na viongozi wa Iran ndiyo
siri ya mafanikio na ushindi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika
kukabiliana na mashinikizo na vitisho vya maadui. Meja Jenerali Muhammad
Ali Jaafari ameongeza kuwa, wananchi wa Iran wamesimama imara kwa lengo
la kuhifadhi thamani za Mapinduzi ya Kiislamu licha ya kuwepo
mashinikizo ya mabeberu wa Magharibi. Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi
wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran amesema, madola ya Magharibi
yamedhoofika na wala hayana uwezo wa kufanya shambulio la kijeshi dhidi
ya Iran na kusisitiza kuwa, SEPAH daima iko imara kwa ajili ya kulinda
ardhi ya Iran mbele ya uchokozi wa aina yoyote ile. Akielezea uchochezi
wa Marekani, utawala wa Kizayuni wa Israel na baadhi ya nchi za eneo la
Mashariki ya Kati wa kuleta ghasia na machafuko nchini Syria, Meja
Jenerali Jaafari ameongeza kuwa, njama za maadui zimegonga za kumng'oa
Rais Bashar Assad pamoja na kusambaratisha muqawama wa wananchi wa
No comments:
Post a Comment