Uungaji mkono kwa bara la Afrika na juhudi za kutatuliwa migogoro
katika nchi zilizokumbwa na migogoro barani humo, ndiyo ajenda kuu ya
kikao cha kwanza cha wakuu wa nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa
Francophone kinachoendelea huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo. Taarifa zinasema kuwa, wakuu wa Francophone
wamejikita zaidi katika kujadili migogoro na machafuko ya kisiasa
yaliyoko barani Afrika. Taarifa kutoka Kinshasa zinasema kuwa, wakuu hao
wameafikiana pia juu ya kutolewa maazimio yenye lengo la kukomesha
mgogoro wa mashariki mwa Kongo, na migogoro mingine ya Mali, Madagascar
na Guinea Bissau. Nchi za Senegal na Vietnam zimetangaza kuwania nafasi
ya kuandaa mkutano ujao wa Francophone hapo mwaka 2014.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment