Naibu Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa
amesema hali ya haki za binadamu nchini Mali si ya kuridhisha na
amelaani hatua ya wanamgambo wenye silaha ya kuwatumia vitani wanawake
na watoto wadogo.
Ivan Simonic amesema, vitendo hivyo haviwezi kukubalika na kusisitiza kuwa mauaji ya askari na raia yanayofanywa na waasi nchini Mali yameongezeka huku haki za wanawake na watoto zikikanyangwa.
Kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyojiri nchini Mali mwezi Machi mwaka huu, machafuko yameshadidi nchini humo huku waasi wakidhibiti maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo. Mauaji, utesaji, ubakaji na kushambulia vituo vya kiutamaduni ni miongoni mwa jinai zinazoshuhudiwa kila uchao kwenye nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

No comments:
Post a Comment