Baba wa marehemu anasimulia mtoto wake alikamatwa siku ya sikukuu
mosi akipeleka ng’ombe wake malishoni na akiwa na pesa shilingi elfu 80
ambazo shilingi elfu 30 alichangiwa na baba yake. Pesa hizo alikusudia
kwenda kununua godoro baada ya kumaliza kufunga ng’ombe wake. Baba mtu
alipomuona mtoto wake nje ameshikwa na polisi wasiopungua 20 alikwenda
kusikiliza kumezidi nini? La haula baba mtu alipigwa na kutakiwa aondoke
mara moja. Baba mtu baada ya kushuhudia mtoto wake akipata kipigo hakua
na cha kufanya aliondoka na kumwacha mtoto wake mikononi mwa askari
hao. Baada ya kufika jioni na kuona mtoto wake hajarejea, baba mtu
alikwenda kituo cha polisi Mwanakwerekwe kumtafuta mtot wake lakini
alimkosa ndipo alipokwenda kito kikuu cha polisi Madema na kumkosa pia.
Ndipo baadae akapokea simu kuwa mtoto wake ameshafariki na yupo chumba
cha kuhifadhia maiti hospitali ya Mnazi mmoja na kumkuta akiwa katika
hali kama hiyo
No comments:
Post a Comment