Kundi la wanamgambo wa ash Shabab nchini Somalia limetishia kufanya mashambulizi dhidi ya Uingereza.
Shirika la Habari la Ufaransa limenukuu
taarifa ya kundi hilo ikisema kuwa: Uingereza lazima ilipe gharama kubwa
za vita vyake dhidi ya Uislamu na kitendo chake cha kumrejesha Sheikh
Abu Hamza wa Uingereza nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ash Shabab
imetishia kufanya mashambulizi makali zaidi dhidi ya London kuliko yale
ya tarehe 7 na 21 Julai 2005.
Itakumbukwa kuwa, miripuko ya mabomu ya
tarehe 7 Julai 2005 ilipelekea watu 52 kuuwa mjini London Uingereza.
Wiki mbili baadaye miripuko mingine minne ya mabomu ilitokea kwenye
mfumo wa usafiri wa umma mjini humo.
Somalia haina serikali kuu tangu mwaka
1991 na tangu wakati huo hadi hivi sasa makundi mbalimbali ya watu wenye
silaha yamekuwa yakijitokeza nchini humo kwa ajili ya kujidhaminia
mambo tofauti.
No comments:
Post a Comment