Mawakili wa mwana wa dikteta wa zamani wa Libya wamesema kuwa
wanahofia iwapo kesi ya Saiful Islam itasikilizwa nchini Libya basi
huenda mteja wao huyo akahukumiwa kunyongwa.
Mawakili hao wamedai kuwa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) inapaswa kuchukua tahadhari kwani suala hilo linaweza kuharibu taswira ya korti hiyo iwapo itaruhusu Saiful Islam ahukumiwe nchini Libya.
Matamshi hayo yametolewa katika kikao cha majaji cha kujadili iwapo mwana huyo wa Gaddafi atahukumiwe nchini Libya au katika mahakama ya The Heague. Hii ni katika hali ambayo mahakimu wa serikali wamesema kuwa, Libya inaweza kudhamini kuhukumiwa kwa uadilifu Saiful Islam katika ardhi ya nchi hiyo.
Mwana huyo wa Gaddafi anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na kuua waandamanaji wa Libya mwanzoni mwa siku za harakati za mapinduzi ya wananchi yaliyopelekea kung'olewa madarakani utawala wa baba yake.

No comments:
Post a Comment