Askari
mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha
FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani
na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku katika eneo
la Bububu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa
na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa
kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya
hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
hiyo Sheikh Farid Hadi usiku wa kuamkia jana.
Kamishna
Mussa amesema Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta watu
waliofanya mauaji ya Coplo Saidi Abdulrahaman ili kuwakamata na
kuwafikisha Mahakamani kama sheria za nchi zinavyowaelekeza.
Amesema
mpaka hivi sasa watu 10 wamekamatwa kwa tuhuma za makosa mbali mbali
yaliyotokana na vurugu za jana na upelelezi wa kujua ukweli juu ya uvumi
wa kutekwa Sheikh Farid unaendelea.
Ameongeza kuwa kutekwa
kwa Sheikh Farid kunatia mashaka kutokana na mazingira ya kutoweka
kwake kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mdogo wake Said Omar Said
ambae alikuwa dereva wake katika hatua za mwisho maeneo ya Mazizini walipokwenda kununua umeme.
“Sheikh
Farid alimuamuru Said amuache katika eneo hilo aende nyumbani kupeleka
umeme na wakati huo akaendelea na mazungumzo na watu wengine walikuwemo ndani ya gari nyengine ndogo ya NOAH ambayo nambari zake hazijajulikana lakini aliporudi kumchukua hakumkuta” alisema Kamishana Mussa.
Amesema fujo hizo zilisababisha hasara kubwa kwa Serikali, Chama tawala na wananchi
ikiwemo kuchoma na kuharibumiundo mbinu ya barabara, kuharibu maskani
za CCM za Kisonge na Muembeladu kwa kuzichoma moto baadhi ya magari
kuvunjwa vioo na kuvunja duka la pombe na kuiba mali iliyokuwemo ndani.
Hata hivyo
amedai hali ya Mji wa Zanzibar kwa sasa ni shwari, wananchi wanaendelea
na shughuli zao kama kawaida na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na
vikosi vyengine vya ulinzi na usalama vitaendelea kuhakikisha amani
inadumu muda wote.
Amewataka
wananchi kuendelea kuwa wavumilivu na kudumisha amani na utulivu katika
maeneo yao, na kutoa taarifa za watu waliohusika na vurugu pamoja na mauaji ya Coplo Said Abdulrahaman.
No comments:
Post a Comment