Sudan na Sudan Kusini zimekubaliana juu ya hatua ya
ubadilishanaji wafungwa wa nchi mbili. Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo
ya Ndani wa Sudan Ibrahim Mahmood Hamid alipokutana na kamishna wa
Sudan Kusini katika masuala ya ujenzi mpya na miundo mbinu mjini
Khartoum. Viongozi hao wawili wamekubaliana kubadilishana wafungwa na
kuwarejesha nchini mwao sambamba na kuhukumiwa kwa mujibu wa hukumu za
nchi hiyo. Katika kikao hicho pia walijadili kuondolewa vizuizi
vilivyopo kwa ajili ya kuwarejesha raia wa Sudan Kusini kutoka nchini
Sudan. Katika kipindi cha kujitenga Sudan Kusini kutoka Sudan kaskazini
tarehe tisa mwezi Juni 2011, zilianza harakati za kuwahamisha raia wa
nchi mbili katika maeneo yao ya asili, suala lililopelekea maelfu ya
raia wa nchi mbili hizo kurejea makwao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment