Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuhusu umasikini
katika nchi za kusini mwa jangwa kubwa la Afrika. David Gressly Mratibu
wa Masuala ya Haki za Binadamu wa nchi za kandokando mwa jangwa la
Sahara wa umoja wa Mataifa ameripoti kuwa, maisha ya watu milioni 50
yako hatarini kutokana na uwezekano wa kupungua mazao ya kilimo mwakani.
Gressly ameongeza kuwa kunyesha mvua katika nchi za
kandokando mwa jangwa la Sahara ni ishara ya kuwepo mazao mazuri mwaka
ujao hata hivyo kupungua kwa mazao na pia kupanda kwa bei za vyakula
kutayaweka hatarini maisha ya watu milioni kumi wa eneo hilo.
Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu katika nchi za kandokando
mwa jangwa la Sahara wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, tayari wameandaa
mpango wa kupunguza lishe duni kwa watoto wa Kiafrika milioni moja. Hii
ni katika hali ambayo, mwaka uliopita watoto laki tano wa Kiafrika
walikuwa wakisumbuliwa na tatizo la lishe duni.
No comments:
Post a Comment