Maelfu ya Waislamu wa Ethiopia wamefanya maandamano makubwa kwenye
miji mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga siasa za serikali ya Adiss Ababa.
Waislamu wa Ethiopia wanaituhumu serikali ya nchi hiyo kwa kuingilia
kati masuala ya dini hiyo na hali kadhalika ikifanya njama za
kuwashinikiza Waislamu wafuate mikikati iliyopangwa na serikali.
Malalamiko ya Waislamu dhidi ya siasa na sera za serikali ya nchi hiyo
yameanza tokea miezi tisa iliyopita. Waandamanaji walilaani vikali
mipango ilyoratibiwa na serikali ya kuwachagulia viongozi wa kidini
kinyume na irada na matakwa ya Waislamu walio wengi nchini humo. Hali
kadhalika waandamanaji wametaka waachiliwe huru vingozi wao
wanaoshikiliwa na vyombo vya dola nchini humo.
No comments:
Post a Comment