
Vijikatuni hivyo vimechapishwa katika jarida la kila wiki la Charlie Hebdo la Ufaransa. Wakati huo huo Jumuiya ya Nchi za Kiarabu imetoa wito kwa Waislamu kote duniani kufanya maandamano makubwa ya amani ya kulaani uchapishaji wa vijikatuni hivyo.
Jarida hilo la Ufaransa limethubutu kufanya kitendo hicho kichafu huku Waislamu wakiendelea kuandamana kote duniani kulaani utengenezaji wa filamu inayomvunjia heshima Mtume SAW huko Marekani.
No comments:
Post a Comment