Maelfu ya Waislamu katika mji wa Dar
es Salaam, Tanzania wameandamana kulaani filamu inayomtusi na kumvunjia
heshima Mtume saw. Waislamu hao waliokuwa wakipiga nara dhidi ya
Marekani waliandamana hapo jana na kutoa tamko dhidi ya wanaoshambulia
na kuudhalilisha Uislamu. Akitoa tamko la Waislamu mwishoni mwa
maandamano hayo, Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu Mkuu wa Shura ya
Maimamu Tanzania, ameitaka serikali ya Tanzania kuzuia mitandao ya
intaneti, DVD na mianya mingine kuonyesha filamu hiyo ya kumvunjia
heshima Mtume, sambamba na kutaka kufungwa ubalozi wa Marekani nchini
humo. Aidha Sheikh Ponda Issa Ponda amesema kuwa, tamko hilo ni la
Waislamu wote wanaompigania Mtume na kwamba, kuanzia sasa Waislamu
wanagomea bidhaa zote zinazotengenezwa na Marekani pamoja na utawala wa
Kizayuni wa Israel. Ameongeza kwamba, ubalozi wa Marekani nchini
Tanzania unapaswa kufungwa mara moja, la sivyo Waislamu wa nchi hiyo
watachukua hatua kali zaidi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment