Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 17, 2012

OIC kukabiliana na dharau dhidi ya Mtume (saw)



Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) watajadili njia za kukabiliana na vitendo vya dharau na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw).
OIC kukabiliana na dharau dhidi ya Mtume (saw)Balozi na mwakilishi wa Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) Hamid Reza Dahqani amesema kuwa mawaziri hao watajadili njia za kukabiliana na dharau na vitendo vya kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu katika mkutano wao wa 39 utakaofanyika nchini Djibouti na ule utakaofanyika katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York.
Ameashiria mikono ya nyuma ya pazia iliyohusika katika kuvunjia heshima matukufu ya Kiislamu na kusema kuwa, Wamagharibi daima wamekuwa wakidai kuwa masuala hayo yanatokana na uhuru wa kusema na kujieleza katika katiba za nchi zao. Dahqani ameongeza kuwa taasisi za kimataifa zinasisitiza juu ya udharura wa kuheshimiwa dini za mbinguni, thamani na itikadi za mataifa mbalimbali lakini inasikitisha kuwa hadi sasa juhudi za jumuiya za kutetea haki za binadamu na jumuiya za kimataifa ikiwemo OIC hazijafanikiwa kuwakinaisha Wamagharibi kuhusun ukweli kwamba uhuru hauna maana ya kuvunjia heshima matukufu ya itikadi za watu wengine.

No comments:

Post a Comment