Wanamgambo wa kundi la al Shabab wa Somalia wamesema kuwa wao ndio
waliomfyatulia risasi na kumuua mbunge wa Somalia hapo jana na kutishia
kumuua kila mbunge wa nchi hiyo. Watu waliokuwa na silaha jana walimuua
kwa kumfyatulia risasi Mustafa Haji Mohamed nje ya nyumba yake baada ya
sala ya Ijumaa. Sheikh Abdiasis Abu Musab msemaji wa oparesheni za
kijeshi wa kundi la wanamgambo wa al Shabab amesema kwa kuhoji kuwa ni
mara ngapi wamewaonya Wasomalia kujiunga na serikali ya kikafiri?
Msemaji wa al Shabab amesema wamemuua mbunge Mustafa na kwamba watawaua
wabunge wote na maafisa wa Somalia. Augustine Mahiga Mjumbe Maalumu wa
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia ameyaelezea mauaji ya
mbunge huyo yaliyofanywa na al Shabab kuwa ni kitendo cha woga
kinachokumbusha changamoto zinazozikabili taasisi mpya na uongozi wa
nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment