Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, September 25, 2012

Mahakama ya Misri yawahukumu kifo magaidi 14



Mahakama ya Misri yawahukumu kifo magaidi 14
Mahakama ya Misri imewahukumu kifo magaidi 14 na wengine wanne kifungo cha maisha jela kwa kosa la kushambulia jeshi na maafisa wa polisi katika rasi ya Sinai.
Watu hao ni wafuasi wa kundi moja la wanamgambo ambao wamepatikana na hatia ya kuwaua maafisa watatu wa polisi, mwanajeshi mmoja na raia katika mashambulizi yaliyofanywa mwezi Juni na Julai mwaka 2011.
Eneo la Sinai la Misri kwa muda mrefu limekuwa likikabiliwa na matatizo ya kiuslama. Mwezi Agosti mwaka huu jeshi la Misri lilianzisha operesheni kali ya kuimarisha usalama kwenye eneo hilo baada ya watu wasiojulikana kuuwa askari 16 wa mpakani wa Misri.

No comments:

Post a Comment