Na Masoud ali…
Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya kiislamu Zanzibar imeendelea na harakati zake za kuitakia mema nchi ya zanzibar ili iweze kuwa na uhuru wa kujiamulia mambo wanayotaka.
Hayo yameeelezwa katika mhadhara uliofanyika magogoni katika msikiti wa msumbiji. kwa upande wake naibu amiri wa jumuiya hiyo sh Azzan bin khalid amesema ni wajibu wa kila muislamu kutekeleza wajibu wa kuletwa duniani ili kuweza kufanikiwa siku ya malipo.
Amewataka wazanzibar kuwa na mshikamano na kuwacha sera za vyama vyao ili kuweza kuondoa dhulma inayofanywa na serikali ya muungano wa tanzania.
Aidha naibu amiri wa jumuiya hiyo amebainisha kuwa muda wa kuikomboa zanzibar kupitia mafunzo ya kiislamu umefika hivyo wazanzibar wanatakiwa wasiogope mbinu na vitisho ambavyo vanatolewa na serikali.
Katika mhadhara huo sh Azzan amelaani vakali vitendo ambavyo vimefanywa na maadui wa uislamu duniani vya kumdhalilisha Mtume Muhammad S.A.W vinavyoongozwa na Marekani na Israel.
Akizungumzia juhudi za Jumuiya katika suala zima la kuitetea Zanzibar amesema ni kumuandikia barua ya wazi yenye kurasa 14 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete inayoelezea mustakbali wa Zanzibar.
Nae sh Mselem amesema kwa walipofikia wazanzibar kwasasa ni vigumu kurudi nyuma katika kudai hadhi ya nchi yao hivyo amesisitiza kwamba juhudi za kuitafutia heshima zanzibar zitaendelea..
Wakati huo huo kumejitokeza kikundi cha watu wasiojuilikana na kuchoma moto maskani ya ccm iliopo kariakoo inayojuilikana kwa jina la Kachorora. wanamaskani hiyo wamehusisha tukio hilo na harakati za jumuiya ya uamsho kwa kuwa tukio hilo limetokea wakati wa kurudi katika mhadhara wao lakin sh mselem kwa niaba ya jumuiya amekanusha dai hilo licha ya kwamba kuna baadhi ya vyombo vya habar haraka vimeihusisha uamsho katika tukio hilo.hivyo ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili Kuweza kuwachukulia hatua za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo.
No comments:
Post a Comment