Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, September 25, 2012

Viongozi wa Sudan na Sudan Kusini wakutana



Viongozi wa Sudan na Sudan Kusini wakutana Viongozi wa Sudan na Sudan Kusini wameanza mazugumzo yao huko Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia lengo likiwa ni kutatua hitilafu za muda mrefu kati ya pande mbili hizo. Rais Omar al Bashir wa Sudan na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir jana walifanya mazungumzo chini ya mashikinizo ya kimataifa
ili kumaliza hitilafu za mpaka kati ya nchi mbili hizo. Msemaji wa pande mbili hizo amesema mazungumzo hayo yamekwenda vizuri na kwamba Rais wa Sudan Kusini anataraji kupatikana natija ya kuridhisha baada ya mazungumzo hayo. Hata hivyo msemaji huyo amesema kwamba bado hitilafu zingalipo na kwamba timu husika katika mazungumzo kati ya Juba na Khartoum zinajaribu kufanya kila linalowezekana ili kupunguza mpasuko uliopo.  

No comments:

Post a Comment