Utawala wa Kizayuni umeziomba Umoja wa Ulaya na Marekani kuisaidia
kifedha Mamlaka ya Ndani ya Palestina ili kuzuia kusambaratika mamlaka
hiyo kutokana na malalamiko ya wananchi katika maeneo ya Palestina.
Gazeti la Kizayuni Maariv imeandika kuwa, Israel ina wasiwasi huu
kwamba, kusambaratika uchumi katika maeneo yanayodhibitiwa na Serikali
ya Ndani ya Palestina kutaibua Intifadha ya tatu ya Wapalestina.
Utawala wa Kizayuni unaamini kuwa, hali mbaya ya kiuchumi katika maeneo
yanayodhibitiwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina itadhoofisha mamlaka
hiyo na idara za usalama za Serikali ya Ndani ya Palestina. Kwa msingi
huo utawala wa Kizayuni umetuma barua za haraka kwa Umoja wa Ulaya na
Marekani ukizitaka pande hizo kuisaidia kifedha Serikali ya Ndani ya
Palestina ili kuzuia
No comments:
Post a Comment