skip to main |
skip to sidebar
Ikhwan: Hakuna mwafaka kati ya Israel na Misri
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ikhwaanul Muslimiin nchini Misri
amesema kuwa, Rais Muhammad Mursi wa nchi hiyo hatakutana na kufanya
mazungumzo na kiongozi yeyote wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Mahmoud
Hussein amesema kuwa, Rais Mursi hatakutana na kiongozi yeyote wa
utawala wa Israel hata kama ikiwa ni kuufanyia marekebisho mkataba wa
amani wa Camp David. Mahmoud Hussein amesisitiza juu ya kukomeshwa
uchokozi unaofanywa na utawala huo ghasibu dhidi ya wananchi wa
Palestina wa eneo la Ukanda wa Gaza, sanjari na kusimamishwa kikamilifu
ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika eneo la Ukingo wa
Magharibi wa Mto Jordan. Katibu Mkuu wa Ikhwaanul Muslimiin amesema,
hakuna kiongozi yeyote wa Misri atakayefanya mazungumzo na kiongozi wa
Israel hadi pale zitakapodhaminiwa haki za wananchi wa Palestina.
No comments:
Post a Comment