Mpaka wa anga kati ya Ivory Coast na Ghana ambao ulikuwa
umefungwa kufuatia mashambulizi ya watu wenye silaha dhidi ya wanajeshi
wa Ivory Coast sasa umefunguliwa. Ofisi ya Rais wa Ivory Coast
imetangaza kuwa mpaka wa anga kati ya nchi hiyo na Ghana umefunguliwa
kuanzia leo. Hata hivyo mpaka wa nchi kavu kati ya nchi mbili hizo ambao
ulifungwa kufuatia mashambulizi hayo umeendelea kufungwa. Serikali ya Ivory Coast imeyahusisha mashambulizi hayo ya karibuni dhidi ya wanajeshi wa nchi hiyo na watu waliokuwa na silaha ambao walivuka mpaka na kuingia Kodivaa kutokea Ghana. Ivory Coast ilifunga mipaka ya anga na nchi kavu kati yake na Ghana tangu Ijumaa iliyopita. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ivory Coast amesema kuwa mashambulizi hayo yamefanywa na wafuasi wa Laurent Gbagbo Rais wa zamani wa nchi hiyo ambao walikimbilia nchini Ghana.

















No comments:
Post a Comment