Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon
imeitisha maandamano makubwa zaidi nchini humo kulaani hatua ya
kuvunjiwa matukufu ya dini ya Kiislamu.
Maandamano hayo yenye lengo la kutetea matukufu ya Kiislamu
yanatarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo mjini Bairut, Lebanon. Hivi
karibuni pia Waislamu mjini Bairut walifanya maandamano makubwa
wakilaani filamu iliyomtusi mtukufu Mtume Muhammad (sww) na kuutaka
ulimwengu wa Kiislamu uchukue hatua kali za kukabiliana na njama za
Marekani. Aidha hapo jana raia mmoja wa Lebanon aliuawa na wengine
kadhaa kujeruhiwa baada ya waandamanaji waliokuwa wamejawa na hasira
kali kutaka kuvamia hoteli moja ya Kimarekani nchini humo. Mbali na
Lebanon nchi nyingine za Kiislamu kamavile Misri, Libya, Bahrain,
Tunisia, Yemen, Iran, Indonesia na Palestina zilishuhudia maandamano
makubwa huku idadi ya watu wakiuawa na kujeruhiwa vibaya.

No comments:
Post a Comment