Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, September 15, 2012

Wanajeshi wa Marekani wawasili San'aa, Yemen



Wanajeshi wa Marekani wawasili San'aa, YemenDuru moja ya kuaminika imeripoti kuwa, wanajeshi wa Marekani wamewasili huko San'aa mji mkuu wa Yemen. Duru hiyo imeripoti kuwa, wanajeshi 150 wa kikosi cha majini wa Marekani wamewasili katika uwanja wa ndege wa San'aa wa nchi hiyo na ndege moja ya kijeshi ya Marekani. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi hao wa Marekani wamewasili huko San'aa Yemen ili kuulinda  ubalozi wa nchi yao na kulinda maslahi ya Washington nchini humo. Mitaa minne inayoelekea katika ubalozi wa Marekani mjini San'aa jana ilishuhudia maandamano makubwa ya Wayemeni dhidi ya Marekani, na baadae maandamano hayo yaligeuka na kuwa ghasia baada ya vikosi vya usalama vya Yemen kuingilia kati na kusababisha raia wanne kuuawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa.
Maandamano hayo yalifanyika kufuatia kutengenezwa filamu huko Marekani inayomvinjia heshima Mtume Muhammad s.a.w. Watu walioshuhudia wameleza kuwa, wanajeshi wa Marekani waliwafyatulia risasi raia wa Yemen  kutokea ndani ya ubalozi na kuwauwa.  Mji wa Taiz pia huko Yemen leo umeshuhudia maandamano makubwa ya wananchi dhidi ya filamu hiyo ya udhalilishaji ya Marekani iliyotengenezwa na Sam Bacile.

No comments:

Post a Comment