Duru za habari kutoka Nigeria zinaarifu kuwa, mafuriko
yaliyosababishwa na kunyesha mvua kubwa tangu mwezi Juni hadi mwezi huu
nchini humo, yamepelekea kuuawa watu 160. Ripoti iliyotolewa na ofisi
inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa Mataifa yenye makao
yake makuu mjini Niamey, Niger imetangaza kuwa, takwimu za hivi karibuni
zinaonyesha kuwa zaidi ya watu laki tano na 27 elfu wameathiriwa na
mafuriko hayo huku watu 81 wakipoteza maisha yao. Awali viongozi Nigeria
walikuwa wametoa ripoti iliyoonyesha kuuawa watu 68 na wengine laki
nne na 85 elfu wakiathiriwa vibaya na mafuriko hayo. Aidha ripoti
iliyotolewa na ofisi inayoshughulikia masuala ya kibinaadmu ya Umoja wa
Mataifa imeashiria kuwa watu wengine 81 wamefariki dunia kwa ugonjwa wa
kipindupindu uliyoyakumba maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo na kufanya
idadi ya watu waliopoteza maisha yao kufikia 160.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment