Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, September 14, 2012

Hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)



Wimbi la malalamiko na hasira za Waislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume Muhammad (saw) linazidi kuenea katika maeneo mbalimbali ya dunia.
Hasira ya ulimwengu wa Kiislamu dhidi ya filamu inayomdhalilisha Mtume (saw)Baada ya mauaji ya balozi wa Marekani na wanadiplomasia wengine watatu wa nchi hiyo katika mji wa Benghazi huko Libya maelfu ya Wamisri waliokuwa na hasira wameendelea kuuzingira ubalozi wa Marekani mjini Cairo kwa siku kadhaa. Wamisri 250 walijeruhiwa baada ya polisi kuingilia kati.
Mjini Sanaa Yemen vijana waliokuwa na hasira jana Alkhamisi walivamia ubalozi wa Marekani na kupanda juu ya ukuta wa uzio wake ambako walitundika juu bendera yenye jina tukufu la Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw). Askari usalama wa Yemen walishambulia maandamano hayo makubwa na kuua watu wanne kati ya waandamanaji hao.
Wananchi wa Saudi Arabia pia wamefanya maandamano katika maeneo tofauti ya nchi hiyo wakilaani filamu ya Kimarekani inayomtusi na kumvunjia heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu. Wasaudia wametoa wito wa kufukuzwa balozi wa Marekani nchini kwao.
Maandamano makubwa kama hayo yamefanyika pia katika nchi za Lebanon, Palestina, Tunisia, Morocco, Pakistan, Afghanistan, Indonesia, Sudan na kwengineko ambako Waislamu wamelaani vikali filamu ya matusi inayomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) iliyotengenezwa na raia wa Marekani na Israel na kufadhiliwa na Mayahudi 100.
Hapa nchini Iran maelfu ya watu walifanya maandamano jana mbele ya ubalozi wa Uswisi unaolinda maslahi ya Marekani mjini Tehran wakitangaza hasira yao dhidi ya filamu hiyo na kutoa wito wa kufikishwa mahakamani na kuadhibiwa wale wote waliohusika kwa njia moja au nyingine katika kutayarisha na kusambaza filamu ya "Innocence of Muslims" Mamilioni ya wananchi wa Iran pia wanatazamiwa kuandamana kote nchini hii leo kabla na baada ya swala ya Ijumaa kulaani filamu hiyo ya Kimarekani.
Wakati huo huo magazeti ya serikali ya China yamelitaja tukio la kuuawa balozi wa Marekani nchini Libya kutokana na hasira za Waislamu dhidi ya filamu hiyo inayovunjia heshima matukufu yao kuwa ni tukio kubwa zaidi baina ya ulimwengu wa Kiarabu na serikali ya Washington tangu ilipoanza harakati ya mwamko wa Kiislamu Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika.
Gazeti la Watu la chama tawala huko China limezungumzia tabia ya Wamarekani ya kuvunjia heshima mara kwa mara ustaarabu na itikadi za Kiislamu na kuandika kuwa, katika miaka ya hivi karibuni Wamarekani wamekuwa wakikariri vitendo vya kuvunjia heshima itikadi na matukufu ya Waislamu ikiwa ni pamoja na kuchoma moto nakala za Qur'ani, suala ambalo lilizusha malalamiko makubwa kote duniani.
Wimbi la sasa la hasira na malalamiko ya Waislamu dhidi ya Marekani lilianza baada ya video yenye dakika 14 ambayo ni sehemu ya filamu iliyopewa jina la "Innocence of Muslims" kusambazwa katika mtandao wa kijamii wa Youtube.
Mtayarishaji wa filamu hiyo ya kudhalilisha ni Sam Bacile ambaye ni raia wa Marekani na Israel. Mzayuni huyo amesema ametayarisah filamu hiyo kwa dola milioni tano zilizotolewa na Mayahidi 100.
Mashambulizi yanayoendelea kufanywa na watu wa dini mbalimbali dhidi ya balozi za Marekani katika Mashariki ya Kati baada ya kuvunjiwa heshima Mtume wa Mwenyezi Mungu yanatoa ujumbe wa wazi kwa viongozi wa White House kwamba, tokea sasa dharau na utovu wa adabu utakaofanywa na Mmarekani mmoja dhidi ya Uislamu hautatambuliwa kuwa ni tendo la mtu binafsi bali litahusishwa na mfumo unaopanga hujuma dhidi ya Uislamu huko Marekani na katika nchi za Magharibi kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment