Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, September 10, 2012

WAZANZIBARI VIJANA, WASOMI TUWASAIDIE UAMSHO.


WAISLAMU WENGINE WAKO WAPI ?
VIJANA TUNA MATATIZO NINI KIFANYIKE
MIKAKATI IANZE TUIGE WENZETU

BY Zdaima
“Hongera Uamsho Hongereni sana Allah atambuwe jitihada zenu na uwezo wenu kwa upande wenu mmeshajitahidi kazi ni kwa vijana wasomi wanaojiita Wazanzibari” ningeanza makala yangu hii kwa salamu hizo.
Naam naandika maelezo yangu haya nikiamini wazalendo mtayasoma kwa umakini mkubwa na mazingatio sana.Si lengo langu kulaumu au kumkwaza mtu .
Tokea kuanza vuguvugu la mabadiliko ya katiba tumeshuhudia mengi mazuri na mabaya kwa hapa kwetu zanzibar. na wengi tumejinasibu kuwa ni wazalendo wa kutaka kuitetea zanzibar kuondokana na kile almaarufu tunachokiita ukoloni wa mtanganyika dhidi ya zanzibar kupitia muungano.Bila shaka hamasa ya kudai mamlaka ya zanzibar yameimarika zaidi baada ya wenzetu ,mashehe wetu kwa umoja wao wa taasisi za kidini hapa zanzibar wakiongozwa na ( JUMIKI) kulivalia njuga bila kutafuna maneno wala kuegemea milengo ya kisiasa ilimuradi lina maslahi na zanzibar. Tunajua harakati za kudai mamlaka ya zanzibar zimeanzia mbali sana na kumetokea mambo mengi zanzibar kwa ufupi wa mambo historia ni ndefu (rejea Mihadhara ya Sheikh Ilunga Hassan) kwenye CDs mbali mbali za Mfumo kristo na muungano.

Ninachotaka kusema ukitoa vijana wa wakati wa zamani walioegemea milengo ya kisiasa jee vijana wa leo wasomi wanaisaidiaje Zanzibar kudai mamlaka yake.? tunajukumu hapa
Vijana tumekuwa ni wadandiaji tu wa hoja na si waanzilishi wa hoja hii imekuwa ndio khulka yetu na tumekuwa mabingwa wa kuwakosowa wengine. Kwa mfano baadhi ya watu wakiwemo vijana wanawakosowa uamsho kila wakifanya initiatives za kudai maslahi ya wazanzibari na katika utamaduni wa zanzibar uheshimiwe huwakosowa kwa kuangalia maslahi ya kisiasa zaidi bila kujali maslahi ya kijamii zaidi ( utamaduni wa jumla wa Zanzibar ( uislamu). Hata iwe wanakosea basi kwa upande wao uwezo wao umefika hapo na jitihada zao zimefika hapo kutetea maslahi ya kitamaduni na kijamii wewe kijana umefanya lipi kusaidia ? Mimi sikatai watu kuwashauri uamsho katika kuboresha hapana lakini nakataa ile khulka ya kupinga bila kutowa suluhisho na kuwaona wao tu ndio wenye jukumu la kuitetea zanzibar na sisi wengine kurukukia rukia tu kwa nini vijana tumeshindwa kuanzisha chombo cha kutuunganisha tukawa kitu kimoja na tukawa mstari wa mbele kuibuwa hoja na kufanya harakati?

MATATIZO YA VIJANA WENGI.
Tumekosa elimu sahihi ya dini. ( Religious Knowledge)
Sitaki kusemea dini nyengine labda nieleze ile inayonihusu ( islamic knowledge) ambapo mazingira nayajua hapa zanzibar. Vijana wengi hatuijui dini yetu na tunashindwa kujuwa wajibu wetu katika kuitetea dini na tamaduni zetu. tunachanganya mambo bila kujuwa mwelekeo wake. tumeathiriwa na urithi wa dini kitu ambacho hakitakiwi katika uislamu. Jee vijana hatuoni yanayofanyika mitaani na majumbani mwetu ikiwa ni waislamu 99% hatukutegemea mambo machafu kwa asilimia 99% mchango wa vijana uko wapi . hata ukisikia panapigwa kelele ni uamsho pekee si wawakilishi wala wabunge na hata hao uamsho hatuoni uwakilishi wa vijana katika safu yao tuko wapi vijana? Inasikitisha vile vile kuwa na wanazuoni wengi katika idara za serikali na wasomi kadhaa wa kiislamu katika nchi hii lakini kiasi cha kushindwa kuitumia elimu yao ya dini angalau kumpanga nesi wa kuchoma sindano mwanamme kuwa mwanamme na mwanamke kuwa mwanamke mweziwe hata hili basi. elimu yetu ya dini haitusaidii kutatuwa matatizo madogo madogo yanayoendana na tamaduni zetu. hivyo hivyo kwa sheria kandamizi .mahkamani na hata usafiri .baadhi ya vitu hata hizo nchi za magharibi wanafanya kwa tamaduni zai ( ukiristo) wala si tatizo. tumekosa elimu sahihi na kujiamini vijana tuna mchango gani?

Uislamu wetu hauna mwelekeo.
Vijana ndio tunaongoza kwa uharibifu wa tamaduni zetu wenyewe. tumekuwa wazuri wa kuiga mabaya na si mema. hatujuwani kuwa na wapenzi wa kike na kiume kinyume cha utaratibu wa dini.VfUTA FIKRA WEWE NI RAFIKI ZAKO WANGAPI WANA GIRL FRIENDS AU BOY FRIENDS, DADA ZAKO NYUMBANI KWENU, NA HATA MWENYEWE VIPI.wavuta bangi, wezi, hawaswali nk. tumesahau wajibu huu na kuuona ni wa uamsho basi hata huu wa kuitetea nchi nao hatuuoni? tumeiga tamaduni za kimagharibi na kujitwishwa halafu tunasema tuna uchungu na nchi hili la kulinda tamaduni za nchi sisi wenyewe kwanza halimo katika uzalendo au si wajibu wetu kama vijana?
Kuegemea siasa na umajimbo.
Tunapenda kujitukuza kwa asili zetu na maeneo yetu kitu ambacho hakitusaidii.tunavunja mshikamano wetu. labda ni sababu za kihistoria lakini kwa nini vijana tunaendeleza historia ambayo inatunyima utengamano wetu. kwa hapa zanzibar kila mmoja na chama chake na kwao.unaonaje tungekuwa na ajenda za kiinchi katika mtazamo wa vijana kisha vijana bila kujali vyama vyao wakaibeba kwa umoja wao na kufanya harakati hasa zile zinazohusu mustakbali wa kiinchi na vijana wajao? jee tuna mawazo angalau ya kuanzisha chombo cha vijanakwa zanzibar. Hivyo vilivyopo viko kimaslahi ama ya kisiasa, au kimapato sio kimamlaka ya nchi na uzalendo.
Mengine.
- Kutojuwa lengo letu kwa wakati fulani
- Kuburuzwa (baadhi)
- Kutojiamini
- Kukosa ujasiri n.k.

TUWAIGE WENZETU.
Mfano mdogo kule bara wenzetu uislamo wao umefika juzi juzi tu lakini kwa wale wanaofuatilia watakubaliana nami kwamba waislamu wa bara wanajitambua zaidi ingawa sio wote hasa vijana na wamekuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii. Hizi harakati zote zinazoendelea chimbuko lake ni kundi la vijana wa miaka ya 80 ambapo harakati zao zilianzia pale UDSM chini ya Professer ( simtaji) kutoka nje aliyewashtuwawaislamu kutoka usingizini . Vijana hawa walileta mwamko wa kielimu kwa waislamu na wakashajiishana kuchukuwa fani mbali mbali ili kuusaidia uislamu hatma yake wakaanzisha maskuli na kupasisha kweli kweli na ndio hizi sisi wazanzibari tunawapeleka watoto wetu. inasikitisha sisi kushindwa kujielewa pamoja na uislamu wetu wa asili kushidwa kuwa na mipango kama vijana. Wenzetu wametumia mtandao wa vijana wasomi kuuelimisha umma wa kiislamu na walianzisha mataasisi mbali mbali na kwa sasa products yake imepatikana vugu vugu la mfumo kristolimeanzia na mkakati wa kuwaelimisha dhima ya vijana wa kiislamu wasomi katika jamii, historia ya ukweli ya tanganyika, nafasi ya waislamu katika serikali yao nk. leo kuna kundi kubwa la vijana wameshaanza kupenya serikalini na huku nje kuna harakati zinaendelea hio ni kazi ya vijana sisi zanzibar kazi na siasa na kujitukuza. Tutumie siasa zetu kama nyenzo kutufikisha kwenye mustakbali vijana tusijisahau.
Kwa mfano hapa zanzibar tuna tatizo la matokeo mabovu kila mwaka na yanaathiri mustakbali wa nchi huko mbele badala ya vijana tukaanzisha forum ya kutatua tatizo hilo labda kwa kuunda mtandao wa vijana zanzibar katika elimu na utaalamu tunasubiri wanasiasa waseme, uamsho waandamane ndio na sisi tuzuke.Huko nyuma tulisikia kuna kundi linaitwa Zanzibar Elite club lilikuwa bale UDSM sasa siwasikii kila mtu na mambo yake ni mifano ya mambo kama haya. tumejisahau inawezekana mfumo wetu wa elimu una matatizo vijana tungesimama kusaidia taifa na jamii tusiwasubiri uamsho au vyama vya siasa ndipo nasi tuunge mkono bila kuwa na mwavuli unaotutambulisha. hata katika uchumi, dini, migogoro nk kwani hakuna wataalamu vijana ? sio ndio wengi ikiwa ni walimu, madaktari, maofisa mbali mbali , wanauchumi, wanasheria n.k. kule bara kuna chombo kinaitwa TAMPRo ( Tanzania Muslim Proffesional ) kina jaribu kuratibu na kushughulikia matatizo ya waislamu. ni chombo kilichowaunganisha wataalamu waislamu kusaidia jamii ya kiislamu na inaongozwa na vijana sisi tumelala.jamaa wanatowa miongozo mbali mbali ya kisheria, kiujasiriamali,taaluma,kibiashara na wanapiga hatua tuwaige kwa yale mazuri wenzetu Zanzibar tumeiacha dini yetu na mifumo yetu na ntumeshindwa kufanya kile kitu kinaitwa ( islamization of Enviroment) na ndio ukakuta wasomi wengi lakini hawana athari katika jamii.
MWISHO.
Vijana wasomi tuujuwe wajibu wetu kuisaidia jamii iwe ni kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi,nk. tuanze sasa nafikiri nitowe changamoto ya kuanzishwa chombo cha kuwaunganisha wazaznibari vijana cha wataalamu kitakachokuwa na mwavuli wa dini ili kuepusha mitafaruku ya kiitikadi na kisiasa. tunaweza tukafika ingawa kuna changamoto ya kiutawala na uwezo wa kifedha . tufikirie hili.
Nawasilisha

No comments:

Post a Comment