Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, September 23, 2012

Wanigeria waandamana kumtetea Mtume SAW



Wanigeria waandamana kumtetea Mtume SAW
Makumi ya maelefu ya watu wamefanya maandamano makubwa katika mji wa pili kwa ukubwa Nigeria wa Kano kulaani vitendo vya kumvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Waandamanaji wametoa nara kama vile ‘Mauti kwa Marekani’, ‘Mauti kwa Israel’ na  ‘Mauti kwa Maadui wa Uislamu’. Mmoja kati ya viongozi wa Harakati ya Kiislamu iliyoandaa maandamano hayo Sheikh Mohammad Turi amesema Waislamu wa Nigeria wamejitokeza kubainisha upinzani wao kwa filamu na vijikatuni vilivyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW.
Nchini Ufaransa jeshi la polisi limewazuia Waislamu kuandamana kupinga kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu. Nchi hiyo ya Ulaya sasa imegeuka na kuwa kitovu cha chuki dhidi ya Uislamu.
Wakati huo huo Waziri wa Reli nchini Pakistan Ghulam Ahmad Bilour amesema atatoa zawadi ya dola $ laki moja kwa yeyote atakayemuua mtengenezaji wa filamu ya hivi karibuni inayomvunjia heshima Mtume SAW.

No comments:

Post a Comment