Kamanda wa waasi wa Syria wanaoungwa mkono wa madola ya kigeni
ameuawa na wafuasi wake wenye silaha waliomgeuka katika mji wa Dara'a.
Rabea Swaidan aliuawa kwenye mji huo kusini mwa Damascus hapo jana na
wafuasi wake wakati walipokuwa wakigombania kugawana vitu walivyopora na
fedha walizopokea kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuendeleza shughuli
zao haramu.
Wakati hayo yakiripotiwa vikosi vya serikali ya Syria vimedhibiti maeneo
zaidi katika mji wa Aleppo yaliyokuwa yakikaliwa na magenge yenye
silaha yanayoungwa mkono na madola ya nje, huku waasi 180 wakiuawa na
wengine 30 kukamatwa. Maeneo hayo yamedhibitiwa katika operesheni kubwa
ya kijeshi ya serikali dhidi ya waasi wanaopigana dhidi ya serikali ya
Rais Bashar al Assad wa Syria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment