Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan anatarajiwa kufanya
mazungumzo ya ana kwa ana na mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir siku ya
Jumapili wakati wa kikao cha mwisho cha pande mbili ambacho kimechukua
muda wa majuma mawili. Kikao hicho kilichowashirikisha wawakilishi
kutoka Juba na Khartoum kililenga kutatua mivutano kati ya serikali
mbili hizo kuanzia suala la ugawanaji sawa wa pato la mafuta hadi kadhia
ya usalama wa mipakani. Mkuu wa timu ya Mazungumzo ya Sudan Kusini,
Pagan Amum amethibitisha kuwa kikao hicho kitafanyika mjini Addis Ababa.
Mjumbe maalum wa Norway huko Sudan na Sudan Kusini, Endre Stiansen
amesema jamii ya kimataifa imefurahishwa na jinsi mazungumzo ya pande
mbili yalivyokwenda ndani ya majuma mawili yaliyopita na kwamba Umoja wa
Mataifa una matumaini ya kusainiwa makubaliano ya kudumu kati ya Sudan
na Sudan Kusini kuhusu usalama wa mpakani wakati wa mkutano wa Jumapili
kati ya Marais Omar al-Bashir na Salva Kiir.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment