Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, November 9, 2014

MSIKITI ULIOSANIFIWA NA WANAWAKE WAPATA SIFA KIMATAIFA

Masjid Shakirin unadhaniwa kuwa msikiti wa kwanza nchini Uturuki kusanifiwa na wanawake na unavutia. Msikiti huo unaopatikana mjini Istanbul unajumuisha usanifu wa kisasa na ule wa kizamani unaotumika katika majengo, misikiti na miradi mingine ya Kiuthmaniya.
Msikiti huo wenye uwezo wa kuchukua watu 500 ulisanifiwa bibi Zeynep Fadıllıoğlu ambaye ni maarufu kwa kusanifu maduka, migahawa na hoteli mbalimbali za kisasa akishirikiana na wataalamu wengine wanawake.
Aidha, msikiti huo unahusisha mtindo wa kiuthmaniya wa zamani unaojumuisha qubah kubwa katika eneo kuu la kuswali, minara na ukumbi mkubwa.















No comments:

Post a Comment