Masjid
Shakirin unadhaniwa kuwa msikiti wa kwanza nchini Uturuki kusanifiwa na
wanawake na unavutia. Msikiti huo unaopatikana mjini Istanbul
unajumuisha usanifu wa kisasa na ule wa kizamani unaotumika katika
majengo, misikiti na miradi mingine ya Kiuthmaniya.
Msikiti huo
wenye uwezo wa kuchukua watu 500 ulisanifiwa bibi Zeynep Fadıllıoğlu
ambaye ni maarufu kwa kusanifu maduka, migahawa na hoteli mbalimbali za
kisasa akishirikiana na wataalamu wengine wanawake.
Aidha, msikiti huo unahusisha mtindo wa kiuthmaniya wa zamani
unaojumuisha qubah kubwa katika eneo kuu la kuswali, minara na ukumbi
mkubwa.