Sunday, December 28, 2014
MISRI NA MOROCCO ZAPIGA MARUFUKU FILAMU INAYOMUONESHA MUNGU
Misri na Morocco zimepiga marufuku filamu iliyotengenezwa Hollywood isioneshwe katika mataifa hayo ya Afrika Kaskazini.
Vyombo vya habari nchini Morocco vimetangaza kuwa mameneja wa sinema katika pembe zote za nchi hiyo wamepewa maagizo ya kutoonesha filamu iliyojaa utata ya “Exodus: Gods and Kings,” kwa sababu “inamuonesha Mungu,” jambo ambalo ni haramu katika Uislamu.
Mapema waziri wa utamaduni wa Misri, Gaber Asfour alisema kuwa filamu hiyo imejaa makosa lukuki ikiwa ni pamoja na madai kwamba “[Nabii] Mussa na Wayahudi ndio waliojenga mapiramidi,” na kuongeza kuwa, “hilo linapingana kabisa na taaarifa za kihistoria zilizothibitishwa”.
Adiha, waziri huyo ameashiria kuwa filamu hiyo iliyoongozwa na Ridley Scott, ni ya kizayuni na imetengenezwa kwa malengo ya kisiasa.
“Inatoa historia kwa mujibu wa uzayuni na ina makosa lukuki ya kihistoria na ndio maana tumeamua kuipiga marufuku”, alisema.
Mapema mwezi Mei, mwandishi na mtunzi maarufu wa filamu Art Olivier alisema kuwa makampuni mengi ya filamu za Hollywood zinamilikiwa na wafanyabishara wa Kizayuni.
Kwa miaka kadhaa Hollywood imekuwa ikitengeneza filamu nyingi zinazolenga kuuchafua Uislamu na Waislamu.
Saturday, December 27, 2014
MAASKOFU WAMPONGEZA RAIS KIKWETE
dar-es-salaam.
maaskofu wa madhehebu mbalimbali za kikristo
nchini wamepongeza uamuzi wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dr jakaya mrisho kikwete wa kuwawajibisha watendaji wake.
wakizungumza kwa mnasaba wa sikukuu ya krismasi
maaskofu hao, wametaka kutoishia
kuchukua hatua kwa waliotajwa kuhusika na sakata la akaunti ya
tegeta escrow pekee, bali kuwachukulia
hatua wazembe na wote wanaokutwa na
tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
naye askofu michael hafidh wa zanzibar amemshauri rais kikwete kuendeleza utaratibu wa kuwawajibisha
viongozi wazembe na wasio waadilifu katika
kazi zao.
BALOZI SEIF AZURU MSIKITI MKONGWE AFRIKA MASHARIKI
ZANZIBAR.
MAKAMU WA
PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ BALOZI
SEIF ALI IDDI AMETEMBELEA MSIKITI MKONGWE ZAIDI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI ULIOPO MICHEWENI
MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
AKISALIMIANA
NA UONGOZI WA KAMATI YA MSIKITI HUO PAMOJA NA BAADHI YA WAANZILISHI WAKE, BALOZI SEIF ALIWAKUMBUSHA WAUMINI
WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUSHIKAMANA KAMA MAAMRISHO YA DINI YAO
YANAVYOELEKEZA.
AMESEMA KUWA
DINI YA KIISLAMU IMEKUWA IKISISITIZA
SUALA LA AMANI, JAMBO AMBALO LITAKAPOFUATWA NA KUTEKELEZWA IPASAVYO HUSAIDIA KUWAPA UTULIVU WANANCHI
KUFANYA IBADA NA SHUGHULI ZAO KAMA
KAWAIDA.
AIDHA BALOZI SEIF AMEWAASA WAISLAM KUWA MAKINI
KATIKA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA BAADHI YA WATU HUSUSAN WANASIASA KUJARIBU KUSHAWISHI WATU
KUFANYA HIVYO, MATOKEO YAKE NI KUANZISHA CHECHE ZA UHASAMA NA WASI WASI KATIKA
JAMII.
MSIKITI WA
IJUMAA WA MICHEWENI MJINI UNAKISIWA KUJENGWA TOKEA KARNE YA 14, KIPINDI AMBACHO
KILIKUWA NA HARAKATI ZA KUSAMBAZWA KWA
DINI YA KIISLAMU KATIKA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI.
Subscribe to:
Posts (Atom)