mahkama kuu vuga mjini zanzibar imeutaka
upande wa mashtaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya ushahidi
vitakavyotumika katika kesi inayowakabili viongozi wa harakati ya jumuiya na taasisi zakiislam
zanzibar .
jaji wa mahkama hiyo fatma hamid mahmoud
ametoa ombi hilo alipokuwa akiendesha kesi inayowakabili viongozi hao
katika mahakam kuu vuga mjini zanzibar .
jaji huyo pia ameutaka upande wa mashtaka
kuwasilisha kwa maandishi sababu za kuzuiya dhamana ya viongozi hao
waliokaa rumande kwa mwaka mmoja sasa.
hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashtaka wa serikali
rashid abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushahidi wa kesi hiyo tayari vimekamilia
hivyo ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vielelezo vya mashahidi.
kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa
wa kesi hiyo abdalla juma ameiomba mahkama kupanga tarehe ya
kusikilizwa kwa kesi hiyo na vielelezo
viwasilishwe mahkamani hapo kutokana na
ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.
hata hivyo upande wa mashitaka haukuwa na
pingamizi na na ombi hilo na umedai kuwa unaiachia mahkama kuamua.
watuhumiwa katika kesi hiyo ni amiri mkuu wa jumuiya ya
maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed mkaazi wa mbuyuni,amiri mkuu wa jumuiya ya
uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem ali mselem mkaazi wa kwamtipura, ustaddh mussa juma
mussa mkaazi wa makadara
wengine ni
maustadh suleiman juma suleiman
mkaazi wa makadara, khamis ali suleiman mkaazi wa mwanakwerekwe, hassan
bakar suleiman mkaazi wa tomondo, ghalib ahmada juma mkaazi wa mwanakwerekwe
,katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh abdallah said mkaazi wa misufini na
fikirini majaliwa fikirini.
mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni
kuharibu mali, uchochezi,ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni
kula njama ya kufanya kosa.
kosa la nne linamkabili mshitakiwa namba nne
al-. naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh azan khalid ( mkaazi wa mfenesini.
ustadh azan khalid hamdan anadaiwa kutoa
maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha
uvunjifu wa amani.
vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika
kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka 2013 katika maeneo mbali mbali katika manispaa ya mji wa
zanzibar.
jaji fatma ameikhirisha kesi hiyo na kutaka
upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo kabla
ya januar 31 mwaka huu.