Shirika la Mpango wa ChakulalaUmoja
wa Mataifa (WFP) limeanza tena kugawa chakula kwa familia za wakimbizi
wa ndani ya nchi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taarifa ya WFP imesema chakula
kitatolewa kwa watu wapatao 100,000 ambao wamepata hifadhi katika uwanja
wa ndege wa Bangui, mjii mkuu wa nchi hiyo iliyokumbwa na vita vya
ndani. Ugawaji huo umeanza tena baada ya kusitishwa kwa wiki tatu
kutokana na hali ya usalama kwenye eneo hilo. WFP inashirikiana na
mashirika kadhaa ya Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali
pamoja na viongozi wa kijamii ili kuhakikisha mazingira yanaruhusu
kusambaza msaada wa chakula na misaada mingine kwa wakimbizi wa ndani.
Wananchi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaituhumu Ufaransa ambayo ni
mkoloni wa zamani wa nchi hiyo kuwa inachochea mapigano hasa uhasama
baina ya Waislamu na Wakristo nchini humo. Jamhuri ya Afrika ya Kati ni
nchi yenye umuhimu mkubwa kwa madola makubwa ulimwenguni kutokana na
kuwa kwake katika kitovu cha bara la Afrika. Nchi hiyo inakodolewa jicho
la tamaa na nchi kubwa duniani kutokana na utajiri mkubwa wa maliasili
za madini kama almasi, urani na dhahabu.
No comments:
Post a Comment