Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, January 9, 2014

Abdiweli Mohamed, rais mpya wa Puntland, Somalia


Abdiweli Mohamed, rais mpya wa Puntland, Somalia
Dakta Abdiweli Mohamed Ali, Waziri Mkuu wa zamani wa Somalia leo amechaguliwa kuwa Rais wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland, baada ya kumshinda mpinzani wake Abdirahman Mohamed Mohamud kwa zaidi ya kura moja, katika uchaguzi huo uliojaa ushindani mkubwa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Puntland, wabunge 66 wa eneo hilo waliochaguliwa na wakuu wa makabila mwezi uliopita, ndio wenye jukumu la kumchagua Rais wa eneo hilo lililoko kaskazini mashariki mwa Somalia.
Tume ya Uchaguzi ya Puntland ilipitisha majina ya wagombea 11 kati ya 15 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, katika eneo hilo lililojitangazia mamlaka ya ndani tokea 1998.
Dakta Abdiweli Mohamed Ali aliwahi kuhudumu nafasi ya Uwaziri Mkuu wa Somalia tangu mwaka 2009 hadi mwaka 2012. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mapigano yaliyoanza mwaka 1991 nchini Somalia baada ya kuangushwa utawala wa Jenerali Muhammad Siad Barre, yalisababisha baadhi ya maeneo ya Somalia kujitangazia mamlaka ya ndani, kama Somaliland na Puntland. 

No comments:

Post a Comment