MAHKAMA KUU VUGA MJINI ZANZIBAR IMEPUNGUZA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA YALIYOKUWA YAKIWAKABILI VIONGOZI JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU ZANZIBAR YA KULIPA SHILINGI MILIONI 25 NA BADALA YAKE SASA ZIMEKUWA ZA MAANDISHI.
JAJI WA MAHKAMA HIYO FATMA HAMID MAHMOUD AMETOA UAMUZI HUO NA KUSEMA KUWA KUTOKANA NA WATUHUMIWA HAO KUKAA NDANI KWA MUDA MREFU MAHAKAMA IMEONA WANA HAKI YA KUPATIWA DHAMANA.
MASHARTI YENYEWE YALIKUWA NI KUTOA FEDHA TASLIM SHILINGI MILIONI 25, KUWA NA WADHAMINI WATATU WAKIWA NI WATUMISHI WA SERIKALI MMOJA WAO AWASILISHE MALI ISIYOHAMISHIKA PAMOJA NA KUTOSAFIRI NJE YA ZANZIBAR.
HATA HIVYO BAADA YA MAOMBI YA WATUHUMIWA WAKIONGOZWA NA MAWAKILI WAO SALUM TOUFIQ JAJI FATMA ALIKUBALI KILA MSHITAKIWA KUJIDHAMINI KWA SHILINGI MILIONI 25 ZA MAANDISHI PAMOJA NA KUWA NA WADHAMINI WAWILI MOJA AKIWA MFANYIKAZI WA SERIKALI NA WA PILI AWASILISHE MALI ISYOHAMISHIKA BADALA YA WADHAMINI WATATU WAFANYAKAZI WA SERIKALI.
WATUHUMIWA HAO NI AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH FARIDI HADI AHMED,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH MSELEM ALI MSELEM, USTADH MUSA JUMA MUSSA,NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AL-USTADH AZAN KHALID HAMDAN,KATIBU WA JUMUIYA YA UAMSHO USTADH ABDALLA SAIDI NA MAUSTADHI SLEIMAN JUMA SLEIMAN, KHAMIS ALI SLEIMAN, HASAN BAKARI SLEIMAN, GHARIBU AHMADA JUMA, NA FIKIRINI MAJALIWA .
MASHTAKA WALIOSOMEWA WASHITAKIWA HAO NI KUHARIBU MALI, UCHOCHEZI,USHAWISHI NA KUHAMASISHA FUJO NA KOSA LA TATU NI KULA NJAMA YA KUFANYA KOSA
KOSA LA NNE LIKIMKABILI MSHITAKIWA NAMBA NNE AZAN KHALID AMBAE ANADAIWA KUTOA MANENO YA MATUSI KWA KAMISHNA WA POLISI VITENDO VINAVYOWEZA KUSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI.
VITENDO HIVYO VINADAIWA KUFANYIKA KATI YA OKTOBA 17,18 NA 19 MWAKA ,2012 KATIKA MAENEO TOFAUTI KATIKA MANISPAA YAA MJI WA ZANZIBA AMBAPO WASHITAKIWA HAO WOTE WALIKANA MAKOSA YOTE HAYO .
KESI HIYO ILIAKHIRISHWA HADI MACH 27 MWAKA HUU KESI HIYO ITAKAPOSIKILIZWA TENA.