Shirika la Kutetea Haki za Binadmu la Human Rights Watch
limeitaka serikali ya Morocco kuamiliana kiubinadamu na wahajiri wa
Kiafrika wanaopita nchini humo. Taarifa iliyotolewa na shirika hilo
imeeleza kuwa, wahajiri wanaopita nchini Morocco wakitokea maeneo ya
kusini mwa jangwa la Sahara na kuelekea barani Ulaya, wanakabiliwa na
vitendo vya kikatili vinavyofanywa na vikosi vya usalama vya nchi hiyo
ikiwa ni pamoja na kupigwa na kuwekwa rumande bila ya kufunguliwa
mashtaka. Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la HRW limeeleza kuwa,
licha ya kufanyiwa marekebisho sheria za wahajiri na wakimbizi nchini
humo, lakini bado vinaendelea kushuhudiwa vitendo visivyo vya kibinadamu
vinavyofanywa na askari usalama dhidi ya wahajiri.
Wimbi kubwa la wahajiri kutoka kusini mwa jangwa la Sahara limekuwa
likipita nchini Morocco na kuelekea Uhispania, lakini limekuwa
likikumbana na mateso wakati wa kuondoka nchini humo. Morocco
inahesabiwa kuwa kivuko muhimu cha wafanya magendo ya dawa za kulevya na
wahajiri haramu ambao hujaribu kuingia Ulaya kinyume cha sheria.
Sunday, December 28, 2014
MISRI NA MOROCCO ZAPIGA MARUFUKU FILAMU INAYOMUONESHA MUNGU
Misri na Morocco zimepiga marufuku filamu iliyotengenezwa Hollywood isioneshwe katika mataifa hayo ya Afrika Kaskazini.
Vyombo vya habari nchini Morocco vimetangaza kuwa mameneja wa sinema katika pembe zote za nchi hiyo wamepewa maagizo ya kutoonesha filamu iliyojaa utata ya “Exodus: Gods and Kings,” kwa sababu “inamuonesha Mungu,” jambo ambalo ni haramu katika Uislamu.
Mapema waziri wa utamaduni wa Misri, Gaber Asfour alisema kuwa filamu hiyo imejaa makosa lukuki ikiwa ni pamoja na madai kwamba “[Nabii] Mussa na Wayahudi ndio waliojenga mapiramidi,” na kuongeza kuwa, “hilo linapingana kabisa na taaarifa za kihistoria zilizothibitishwa”.
Adiha, waziri huyo ameashiria kuwa filamu hiyo iliyoongozwa na Ridley Scott, ni ya kizayuni na imetengenezwa kwa malengo ya kisiasa.
“Inatoa historia kwa mujibu wa uzayuni na ina makosa lukuki ya kihistoria na ndio maana tumeamua kuipiga marufuku”, alisema.
Mapema mwezi Mei, mwandishi na mtunzi maarufu wa filamu Art Olivier alisema kuwa makampuni mengi ya filamu za Hollywood zinamilikiwa na wafanyabishara wa Kizayuni.
Kwa miaka kadhaa Hollywood imekuwa ikitengeneza filamu nyingi zinazolenga kuuchafua Uislamu na Waislamu.
Saturday, December 27, 2014
MAASKOFU WAMPONGEZA RAIS KIKWETE
dar-es-salaam.
maaskofu wa madhehebu mbalimbali za kikristo
nchini wamepongeza uamuzi wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania dr jakaya mrisho kikwete wa kuwawajibisha watendaji wake.
wakizungumza kwa mnasaba wa sikukuu ya krismasi
maaskofu hao, wametaka kutoishia
kuchukua hatua kwa waliotajwa kuhusika na sakata la akaunti ya
tegeta escrow pekee, bali kuwachukulia
hatua wazembe na wote wanaokutwa na
tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
naye askofu michael hafidh wa zanzibar amemshauri rais kikwete kuendeleza utaratibu wa kuwawajibisha
viongozi wazembe na wasio waadilifu katika
kazi zao.
BALOZI SEIF AZURU MSIKITI MKONGWE AFRIKA MASHARIKI
ZANZIBAR.
MAKAMU WA
PILI WA RAIS WA ZANZIBAR AL-HAJJ BALOZI
SEIF ALI IDDI AMETEMBELEA MSIKITI MKONGWE ZAIDI KATIKA UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI ULIOPO MICHEWENI
MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
AKISALIMIANA
NA UONGOZI WA KAMATI YA MSIKITI HUO PAMOJA NA BAADHI YA WAANZILISHI WAKE, BALOZI SEIF ALIWAKUMBUSHA WAUMINI
WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUSHIKAMANA KAMA MAAMRISHO YA DINI YAO
YANAVYOELEKEZA.
AMESEMA KUWA
DINI YA KIISLAMU IMEKUWA IKISISITIZA
SUALA LA AMANI, JAMBO AMBALO LITAKAPOFUATWA NA KUTEKELEZWA IPASAVYO HUSAIDIA KUWAPA UTULIVU WANANCHI
KUFANYA IBADA NA SHUGHULI ZAO KAMA
KAWAIDA.
AIDHA BALOZI SEIF AMEWAASA WAISLAM KUWA MAKINI
KATIKA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA BAADHI YA WATU HUSUSAN WANASIASA KUJARIBU KUSHAWISHI WATU
KUFANYA HIVYO, MATOKEO YAKE NI KUANZISHA CHECHE ZA UHASAMA NA WASI WASI KATIKA
JAMII.
MSIKITI WA
IJUMAA WA MICHEWENI MJINI UNAKISIWA KUJENGWA TOKEA KARNE YA 14, KIPINDI AMBACHO
KILIKUWA NA HARAKATI ZA KUSAMBAZWA KWA
DINI YA KIISLAMU KATIKA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI.
Sunday, November 9, 2014
MSIKITI ULIOSANIFIWA NA WANAWAKE WAPATA SIFA KIMATAIFA
Masjid
Shakirin unadhaniwa kuwa msikiti wa kwanza nchini Uturuki kusanifiwa na
wanawake na unavutia. Msikiti huo unaopatikana mjini Istanbul
unajumuisha usanifu wa kisasa na ule wa kizamani unaotumika katika
majengo, misikiti na miradi mingine ya Kiuthmaniya.
Msikiti huo
wenye uwezo wa kuchukua watu 500 ulisanifiwa bibi Zeynep Fadıllıoğlu
ambaye ni maarufu kwa kusanifu maduka, migahawa na hoteli mbalimbali za
kisasa akishirikiana na wataalamu wengine wanawake.
Aidha, msikiti huo unahusisha mtindo wa kiuthmaniya wa zamani
unaojumuisha qubah kubwa katika eneo kuu la kuswali, minara na ukumbi
mkubwa.
Saturday, July 12, 2014
PRAY FOR GAZA
Nothing is new in the sixth day of Israeli aggression on the Gaza Strip; just more destruction in civilians houses |
I know that I DON'T have home now! But at least I have my bicycle to play on the ruin of my home . We Palestinian teach life to the whole world |
Thursday, March 27, 2014
KESI YA UAMSHO YAHAIRISHWA HADI JULIA 3
na harith
subeit
zanzibar.
kesi inayowakabili viongozi wa jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar imeakhirishwa hadi julai 3 mwaka huu ambapo imewekewa pingamizi na mkurugenzi wa mashtaka kuhusu dhamana iliyotolewa kwa washtakiwa hao.
mapema muendesha mashitaka kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashitaka dpp raya mselem aliwasilisha pingamizi ya kupinga uamuzi wa mahkama kuu kusikiliza ombi la dhamana ya watuhumiwa hao.
licha ya mahakama kuu kutoa dhamana kwa watuhumiwa bado upande wa mashtaka unapinga suala hilo na umeamua kukata rufaa ili washtakiwa warejeshwe tena rumande baada yakukaa ndani mwaka mmoja na miezi minne.
hata hivyo wakili wa upande wa utetezi abdalla juma ameiomba mahkama hiyo kuakhirisha shauri hilo hadi mahakama ya rufaa itakapokaa na kusikiliza rufaa hiyo.
hata hivyo jaji isack sepetu hakupingana na hoja hiyo.
watuhumiwa waliofika mahakamani leo ni pamoja na amiri mkuu wa jumuiya ya maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed,amiri mkuu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem bin aly, naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar zanzibar al-ustadh azan khalid hamdan.
wengine ni katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh abdalla saidi, maustadh mussa juma mussa, suleiman juma sleiman, khamis ali sleiman, hassan bakari sleiman, gharibu ahmada juma, na majaliwa fikirini majaliwa.
mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni kuharibu mali, uchochezi,ushawishi , kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni kula njama ya kufanya kosa
kosa la nne likimkabili mshitakiwa namba nne al-ustadh azan khalid ambae anadaiwa kutoa maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinaweza v kusababisha uvunjifu wa amani.
vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka ,2012 katika maeneo tofauti katika manispaa yaa mji wa zanziba ambapo washitakiwa hao wote wamekana makosa yote hayo.
viongozi hao walipewa dhamana na mahakama kuu ya zanzibar tarehe 27 mwezi wa pili mwaka huu baada yakutekeleza masharti yaliyowekwa.

Thursday, February 27, 2014
UAMSHO WAACHIWA KWA DHAMANA
MAHKAMA KUU VUGA MJINI ZANZIBAR IMEPUNGUZA MASHARTI MAGUMU YA DHAMANA YALIYOKUWA YAKIWAKABILI VIONGOZI JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU ZANZIBAR YA KULIPA SHILINGI MILIONI 25 NA BADALA YAKE SASA ZIMEKUWA ZA MAANDISHI.
JAJI WA MAHKAMA HIYO FATMA HAMID MAHMOUD AMETOA UAMUZI HUO NA KUSEMA KUWA KUTOKANA NA WATUHUMIWA HAO KUKAA NDANI KWA MUDA MREFU MAHAKAMA IMEONA WANA HAKI YA KUPATIWA DHAMANA.
MASHARTI YENYEWE YALIKUWA NI KUTOA FEDHA TASLIM SHILINGI MILIONI 25, KUWA NA WADHAMINI WATATU WAKIWA NI WATUMISHI WA SERIKALI MMOJA WAO AWASILISHE MALI ISIYOHAMISHIKA PAMOJA NA KUTOSAFIRI NJE YA ZANZIBAR.
HATA HIVYO BAADA YA MAOMBI YA WATUHUMIWA WAKIONGOZWA NA MAWAKILI WAO SALUM TOUFIQ JAJI FATMA ALIKUBALI KILA MSHITAKIWA KUJIDHAMINI KWA SHILINGI MILIONI 25 ZA MAANDISHI PAMOJA NA KUWA NA WADHAMINI WAWILI MOJA AKIWA MFANYIKAZI WA SERIKALI NA WA PILI AWASILISHE MALI ISYOHAMISHIKA BADALA YA WADHAMINI WATATU WAFANYAKAZI WA SERIKALI.
WATUHUMIWA HAO NI AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR SAMAHATU SHEIKH FARIDI HADI AHMED,AMIRI MKUU WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR FADHILATU SHEIKH MSELEM ALI MSELEM, USTADH MUSA JUMA MUSSA,NAIBU AMIRI WA JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YAKIISLAM ZANZIBAR AL-USTADH AZAN KHALID HAMDAN,KATIBU WA JUMUIYA YA UAMSHO USTADH ABDALLA SAIDI NA MAUSTADHI SLEIMAN JUMA SLEIMAN, KHAMIS ALI SLEIMAN, HASAN BAKARI SLEIMAN, GHARIBU AHMADA JUMA, NA FIKIRINI MAJALIWA .
MASHTAKA WALIOSOMEWA WASHITAKIWA HAO NI KUHARIBU MALI, UCHOCHEZI,USHAWISHI NA KUHAMASISHA FUJO NA KOSA LA TATU NI KULA NJAMA YA KUFANYA KOSA
KOSA LA NNE LIKIMKABILI MSHITAKIWA NAMBA NNE AZAN KHALID AMBAE ANADAIWA KUTOA MANENO YA MATUSI KWA KAMISHNA WA POLISI VITENDO VINAVYOWEZA KUSABABISHA UVUNJIFU WA AMANI.
VITENDO HIVYO VINADAIWA KUFANYIKA KATI YA OKTOBA 17,18 NA 19 MWAKA ,2012 KATIKA MAENEO TOFAUTI KATIKA MANISPAA YAA MJI WA ZANZIBA AMBAPO WASHITAKIWA HAO WOTE WALIKANA MAKOSA YOTE HAYO .
KESI HIYO ILIAKHIRISHWA HADI MACH 27 MWAKA HUU KESI HIYO ITAKAPOSIKILIZWA TENA.
Tuesday, February 25, 2014
TIZAMA PICHA:Maelfu ya wananchi wa mkoa wa Hiraan wajitokeza na kupinga Wanajeshi wa Ehiopia.
Maandamano
hayo yalikuwa ya kupinga uingiliaji kati na uchokozi ulio wa wazi wa
Serikali ya Ethiopia dhidi ya Ardhi ya Kislaam ya Somalia.
Kwenye
Barabara ya mji wa Buula Barde walionekana mamia ya Wananchi waliokuwa
wakipita kweye Barabara hizo huko wakitamka maneno dhidi ya Adui asilia
ya Uvamizi wa Ethiopia aliyovishwa vazi la AMISOM.
Wazee
wa koo wa Mkoa wa Hiraan,wanataaluma,walizungumza kwenye Maandamano
hayo na kusema kuwa watakuwa tayari kuingia vita itakayochukua muda
mrefu dhidi ya wanajeshi wa Ethiopia ili kuilinda Dini na Ardhi
yao,waandamanaji wote hao waliokuwa wakipinga Wanajeshi wa Ethiopia kwa
ujumla wamekubaliana kuwa Uingiliaji wa Ethiopia uliokuja na sura mpya
hautoweza kuathiri chochote harakati iliyokuwa ikiendelea dhidi ya
Maadui wa Kigeni walioivamia Rdhi ya Kislaam ya Somalia.
Tuesday, February 11, 2014
Jeshi la Syria lasisitiza kupambana na magaidi
Mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama nchini Syria amesisitiza
juu ya kutiwa mbaroni wale wote waliohusika na mauaji ya halaiki ya
wananchi wasiopungua 71 wa Syria hapo jana. Mkuu wa majeshi ya Syria
ameongeza kuwa, serikali ya Damascus inafanya juhudi za kutatua mateso
yanayowakabili wananchi zinazosababishwa na njama za baadhi ya mataifa
ya nchi za Magharibi na vibaraka wao walioko katika eneo la Mashariki
ya Kati. Mkuu wa Majeshi ya Syria amesisitiza kuwa, jeshi la nchi hiyo
litaendelea kupambana kikamilifu na kuhakikisha kwamba watenda jinai wa
kundi la al Nusra wanahilikishwa kikamilifu.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, magaidi walioko nchini Syria, baada ya kukiteka kijiji cha Maan kilichoko Hamah magharibi mwa Syria waliwauwa kwa halaiki watu 71 wakiwemo wanajeshi 50 wa serikali ya Syria. Mauaji hayo yanatokea katika hail ambayo, leo hii inaanza duru ya pili ya mazungumzo kati ya ujumbe wa serikali ya Syria na wapinzani huko Uswisi.

Ulaya kutuma wanajeshi 500 Jamhuri ya Afrika ya Kati
Mawaziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa nchi wanachama wa Umoja wa
Ulaya wamepitisha mpango wa kupelekwa wanajeshi 500 wa umoja huo huko
Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa lengo la kusaidiana na vikosi vya nchi za
Kiafrika na vile vya Ufaransa katika kuleta amani nchini humo.
Catherine Ashton Mkuu wa Siasa za Kigeni wa Umoja wa Ulaya amesema kuwa,
lengo la kutumwa wanajeshi hao ni kutekelekeleza operesheni za
kukomesha machafuko na mauaji dhidi ya wananchi wa nchi hiyo na hasa
Waislamu ambao wamekuwa wakilengwa na mashambulio ya wanamgambo wa
Kikristo wa Anti Balaka. Siku ya Jumapili iliyopita, Shirika la
Kutetea Haki za Bindamu la Human Rights Watch HRW lilitahadharisha kuwa, machafuko yanaondelea kushuhudiwa nchini humo yatasababisha Waislamu wote kuwa wakimbizi. Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, karibu watu milioni mbili wanahitaji misaada ya kibinadamu nchini humo.

Ikhwanul Muslimin ya Misri yakadhibisha kuunda jeshi
Kiongozi mmoja mwandamizi wa harakati ya Ikhwanul Muslimiin ya
Misri amesema kuwa, harakati za kundi hilo zitaendelea kuendeshwa kwa
njia za amani na kusisitiza kwamba kundi hilo halina mpango kabisa wa
kuanzisha tawi la kijeshi.
Muhammad Ali Beshr amekadhibisha vikali taarifa zilizotolewa na serikali ya Misri kwa vyombo vya habari kwamba, harakati ya Ikhwanul Muslimin imeanzisha tawi la kijeshi kwa lengo la kupambana na polisi na jeshi la nchi hiyo. Kiongozi huyo mwandamizi wa Ikhwanul Muslimiin amesisitiza kuwa, harakati hiyo itaendelea kupigania haki zake zote kwa njia za amani. Inafaa kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni kundi la watu waliobeba silaha lilishambulia kituo cha polisi na kuwauwa askari watano na wengine wawili kujeruhiwa. Serikali ya Misri ililifungamanisha shambulio hilo na kundi la Ikhwanul Muslimiin. Wakati huohuo, Mahakama moja nchini Misri imetoa hukumu ya adhabu ya kifo kwa watu 14 na wengine wanne kifungo cha maisha jela, kwa tuhuma eti walishiriki katika shambulio dhidi ya kituo cha polisi nchini humo.

Friday, January 17, 2014
kesi inayowakabili viongozi wa harakati ya jumuiya na taasisi zakiislam zanzibar .
mahkama kuu vuga mjini zanzibar imeutaka
upande wa mashtaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya ushahidi
vitakavyotumika katika kesi inayowakabili viongozi wa harakati ya jumuiya na taasisi zakiislam
zanzibar .
jaji wa mahkama hiyo fatma hamid mahmoud
ametoa ombi hilo alipokuwa akiendesha kesi inayowakabili viongozi hao
katika mahakam kuu vuga mjini zanzibar .
jaji huyo pia ameutaka upande wa mashtaka
kuwasilisha kwa maandishi sababu za kuzuiya dhamana ya viongozi hao
waliokaa rumande kwa mwaka mmoja sasa.
hatua hiyo imekuja baada ya mwendesha mashtaka wa serikali
rashid abdalla kudai kuwa vielelezo vya ushahidi wa kesi hiyo tayari vimekamilia
hivyo ipangiwe tarehe nyengine ili kuwasilisha vielelezo vya mashahidi.
kwa upande wake wakili anaesimamia watuhumiwa
wa kesi hiyo abdalla juma ameiomba mahkama kupanga tarehe ya
kusikilizwa kwa kesi hiyo na vielelezo
viwasilishwe mahkamani hapo kutokana na
ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.
hata hivyo upande wa mashitaka haukuwa na
pingamizi na na ombi hilo na umedai kuwa unaiachia mahkama kuamua.
watuhumiwa katika kesi hiyo ni amiri mkuu wa jumuiya ya
maimamu zanzibar samahatu sheikh farid hadi ahmed mkaazi wa mbuyuni,amiri mkuu wa jumuiya ya
uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar fadhilatu sheikh mselem ali mselem mkaazi wa kwamtipura, ustaddh mussa juma
mussa mkaazi wa makadara
wengine ni
maustadh suleiman juma suleiman
mkaazi wa makadara, khamis ali suleiman mkaazi wa mwanakwerekwe, hassan
bakar suleiman mkaazi wa tomondo, ghalib ahmada juma mkaazi wa mwanakwerekwe
,katibu wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh abdallah said mkaazi wa misufini na
fikirini majaliwa fikirini.
mashtaka waliosomewa washitakiwa hao ni
kuharibu mali, uchochezi,ushawishi na kuhamasisha fujo na kosa la tatu ni
kula njama ya kufanya kosa.
kosa la nne linamkabili mshitakiwa namba nne
al-. naibu amiri wa jumuiya ya uamsho na mihadhara yakiislam zanzibar al-ustadh azan khalid ( mkaazi wa mfenesini.
ustadh azan khalid hamdan anadaiwa kutoa
maneno ya matusi kwa kamishna wa polisi vitendo vinavyoweza kusababisha
uvunjifu wa amani.
vitendo hivyo vinadaiwa kufanyika
kati ya oktoba 17,18 na 19 mwaka 2013 katika maeneo mbali mbali katika manispaa ya mji wa
zanzibar.
jaji fatma ameikhirisha kesi hiyo na kutaka
upande wa mashitaka kuwasilisha vielelezo na maelezo ya kesi hiyo kabla
ya januar 31 mwaka huu.
Subscribe to:
Posts (Atom)