Rwanda imekataa kutoa viza kwa
maafisa wawili wa timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa iliyoituhumu
Kigali mwaka jana kuwa inawapa silaha waasi wa mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kuwataja kuwa watu wenye upendeleo.
Friday, March 29, 2013
Monday, March 25, 2013
Uamsho haina account wala page facebook
Masoud Khamis Al-Bimani
Jumuia ya UAMSHO na Mihadhara ya Kiislam Zanzibar haina account wala
page ya Facebook, lakini kuna watu kwa makusudi wameamua kutengeneza
Page ya Uamsho hapa FB, kwa lengo la kuitia Doa jumuiya, anakua anapost
vitu visivyo na Maana, kwa lengo la kuupotosha Umma tujihadhari na watu
hawa.
Kesi ya Uamsho yasomwa upya, yapangiwa Jaji Fatma
KESI ya jinai inayowakabili viongozi wa Dini wa Jumuiya ya Uwamsho na
Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) imeanza kusomwa upya leo katika Mahakama Kuu ya Zanzibar baada ya maamuzi ya awali kutenguliwa.
Kesi hiyo namba 9 ya mwaka 2012 ilisomwa mbele ya Jaji Fatma Hamid
Mahmoud na Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Ramadhan Nassib, ambae
aliwataja washitakiwa hao kuwa ni Farid Hadi Ahmed (41) mkaazi wa Mbuyuni,
Wednesday, March 20, 2013
Al Qaeda wamuua mateka wa Kifaransa
Mtandao wa al Qaeda wa kaskazini mwa
Afrika umetangaza kuwa umemuua mateka wa Kifaransa katika kulipiza
kisasi uingiliaji wa kijeshi wa Ufaransa nchini Mali. Mateka huyo wa
Kifaransa kwa jina la Phillippe Verdon alikatwa kichwa na mtandao huo wa
al Qaida tarehe kumi mwezi huu katika kile kundi hilo lilichokisema
kuwa ni kulipiza kisasi cha mashambulizi yaliyoanzishwa na Paris huko
Mali. Verdon alikuwa mmoja kati ya raia wawili wa Ufaransa waliotekwa
nyara mwezi Novemba mwaka juzi huko kaskazini mwa Mali katika mji wa
Hombori.
Polisi ya Misri yamtia mbaroni binamu wa Gaddafi
Polisi ya Misri imesema kuwa imemtia
mbaroni binamu na aliyekuwa mpambe wa karibu wa Muammar Gaddafi
kiongozi wa zamani wa Libya. Hapo jana maafisa wa Misri walisema kuwa
Ahmed Gaddaf al Dam alitiwa nguvuni baada ya vikosi vya usalama
kuizingira nyumba yake katika kitongoji cha Zamalek huko Cairo. Afisa
mmoja wa Misri amesema kuwa afisa huyo wa zamani wa intelijinsia wa
utawala wa Gaddafi atakabidhiwa kwa maafisa wa Libya hivi karibuni.
Baada ya kuzingirwa nyumba yake kwa masaa kadhaa huko katikati mwa
Cairo, binamu huyo wa Muammar Gaddafi alisikika akizungumza na kanali
moja ya televisheni kwa njia ya simu na hapa ninamnukuu" tulifika hapa
kwa mwaliko wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na baraza la kijeshi,
sisi si magaidi wa kuweza kushambuliwa namna hii," mwisho wa kumnukuu.
Tuesday, March 19, 2013
37 wafariki dunia katika ajali ya basi India

Polisi ya India imeeleza kuwa, ajali hiyo mbaya imetokea mapema leo alfajiri katika wilaya ya Maharashtra. Polisi ya Usalama barabarani nchini India imeeleza kuwa, basi hilo lilikuwa likitokea katika mji wa Goa na kuelekea Mumbai; na kwamba dereva wa basi hilo alishindwa kulidhibiti na kutumbukia mtoni. Polisi imeeleza kuwa, ajali hiyo imetokea umbali wa kilomita 350 kusini mwa Mumbai.
Polisi imeeleza kuwa, watu wasiopungua 17 wamejeruhiwa akiwemo dereva wa basi hilo, ambaye hali yake imeelezwa kuwa ni mahututi. Taarifa za awali zinasema kuwa, ndani ya basi hilo kulikuwa na idadi kadhaa ya watalii kutoka nje ya nchi hiyo.
Siasa za Wamagharibi ni za kindumakuwili
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ukombozi ya Bahrain amezikosoa vikali
siasa za kindumakuwili za Magharibi kuhusiana na matukio ya kieneo na
ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Bahrain unaofanywa na
utawala wa Aal Khalifa wa nchi hiyo.
Saeed al Shahabi ameongozana na maelfu ya wapinzani wa Bahrain na kukusanyika mbele ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza mjini London na kusema kuwa, uungaji mkono wa kibubusa wa Marekani na Uingereza kwa utawala wa Aal Khalifa umesababisha utawala huo kuvimba kichwa na kupuuza misingi ya haki za binadamu.
Ameongeza kuwa, siasa za kindumakuwili za nchi za Magharibi sio za kikhlaki na amebainisha kuwa, Washington na London zinapaswa kukomesha uungaji mkono wao kwa utawala wa Bahrain ambao unatenda jinai za mauaji, kuwafunga na kuwashikilia korokoroni wanaharakati na kuwatesa wananchi wa nchi hiyo wanaume na wanawake.

Boko Haram waua walimu watatu Nigeria

Wazimbabwe waipigia kura ya ndio katiba mpya
Matokeo yasiyo rasmi ya kura ya maoni ya katiba mpya nchini
Zimbabwe, yanaonyesha kwamba, wananchi wameipigia kura ya ndio katiba
hiyo ambayo inapunguza madaraka ya rais wa baadaye wa nchi hiyo. Ripoti
zilizosambazwa leo kutoka vituo vya kuhesabu kura, zinaonyesha kuwa,
watu milioni tatu na laki moja kati ya watu milioni tatu na laki nne
waliofika kwenye vituo vya kupigia kura nchini humo, wameipigia kura ya
ndio katiba mpya ya nchi hiyo ya kusini mwa Afrika inayokabiliwa na
mgogoro mkubwa wa kiuchumi. Gazeti la Herald limeripoti kuwa, watu laki
mbili wameipigia kura ya hapana katiba hiyo. Kwa mujibu wa takwimu rasmi
za nchi hiyo, Wazimbabwe milioni sita pekee ndio waliokamilisha
masharti ya kupiga kura nchini. Ilitarajiwa kuwa, hadi kufikia jioni ya
leo, Tume ya Uchaguzi nchini humo ingekuwa imekamilisha kazi za kuhesabu
kura na kutangaza matokeo rasmi ya kura hiyo.
Mapigano kati ya jeshi na waasi Sudan Kusini

Monday, March 18, 2013
Watu 10 wauawa kwenye mlipuko nchini Somalia
Habari kutoka Mogadishu, mji mkuu wa Somalia zinasema kuwa, kwa
akali watu 10 wamefariki dunia na makumi ya wengine kujeruhiwa kufuatia
mlipuko mkubwa wa bomu uliotokea karibu na ukumbi wa kitaifa wa michezo
ya kuigiza.
Habari zaidi zinasema kuwa, bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye gari na kwamba Mkuu wa Usalama wa Mogadishu ndiye alikuwa mlengwa mkuu. Haijabainika wazi iwapo mkuu huyo ameuawa au la.
Kundi la wanamgambo la Al-shabab tayari limedai kuhusika na shambulio hilo. Kundi hilo limeapa kumuondoa madarakani Rais Hassan Sheikh Mohamud, aliyechaguliwa na bunge la Somalia mwaka uliopita. Hii ni katika hali ambayo, wanamgambo hao wanaripotiwa kuuteka mji wa Hudur wa kusini mwa Somalia.

Subscribe to:
Posts (Atom)