Rais Yahya Jammeh wa Gambia amezikosoa vikali nchi za Magharibi
kwa kufanya mauaji ya raia wasio na hatia katika nchi mbalimbali za
dunia kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. Rais Jammeh aliyasema hayo
wakati akiwahutubia wakazi wa eneo la pwani la magharibi ya nchi hiyo
na kuongeza kuwa, vita vya nchi za Magharibi dhidi ya ugaidi ni vita
dhidi ya raia wasio na hatia. Akiashiria mauaji ya ndege za Marekani
zisizo na rubani na mauaji yanayofanywa dhidi ya watu wanaodhaniwa tu
kuwa ni magaidi, Rais Jammeh amesema, kwa hakika Magharibi wanafanya
mauaji ya raia wasio na hatia duniani. Aidha amesisitiza kuwa, watu
wengi wanaouliwa na ndege hizo za kigaidi zisizo na rubani si magaidi na
kwamba, madai ya madola hayo ya kibeberu ya kupambana na ugadi hayana
ukweli wowote na yamejaa upotoshaji.
Kwa uchache watu watatu wanahofiwa kuuawa katika mlipuko wa bomu
uliotokea mjini Arusha nchini Tanzania Jumamosi jioni katika mkutano wa
kampeni wa chama kikuu cha upinzani Chadema.
Hujuma hiyo ya kigaidi ilijiri karibu saa 12 jioni kabla ya
mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe kumaliza kuhutubia wafuasi wa chama
hicho katika Viwanja vya Soweto mjini Arusha. Msemaji wa Jeshi la Polisi
Tanzania Advera Senso amesema uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.