Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, June 14, 2012

Haki Za Mume Juu Ya Mke

حق الزوج على زوجته
Haki Za Mume Juu Ya Mke

بسم لله الرحمن الرحي
Waja wa Allaah! Ninawausia baada ya kuiusia nafsi yangu kumcha Allaah, ndiyo zawadi yetu ya kukutana na Allaah.Anasema Allaah (Ta´ala):
وَتَزَوَّدُواْ فَإِنَّ خَيْرَ الزَّادِ التَّقْوَى وَاتَّقُونِ يَا أُوْلِي الأَلْبَابِ
“Na jitengezeeni zawadi. Na hakika bora yazawadi ni ucha Mungu. Na nicheni Mimi, enyi wenye akili!” (02:197)
Na anasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
"Muogope Allaah popote ulipo, na lifutishe ovu [baya] kwa jema, na tangamana na watu kwa tabia zilizo njema."
Waja wa Allaah! Nifuateni tuzungumzie haki hizi zenye baraka, haki za ndoa
ambazo zimekuja katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume ( صلى لله عليه
وسلم ). Ambazo lau kila mmoja katika mwanandoa angezitekeleza wangeliishi
katika upendo, rahmah, mawada na saada.
Mizozo ilioko kwa wanandoa wengi, chanzo ni kuwa mbali na Shari´ah ya Allaah (´Azza wa Jalla), pamoja na kuiga kichwa mchunga makafiri mulhid wa magharibi.
Waja wa Allaah! Hakika haki za kindoa zimegawanyika aina tatu: 1- Haki ambazo ni wajibu kwa mume juu ya mke wake. 2- Haki ambazo ni wajibu kwa mke juu ya mume wake. 3- Na haki ambazo wanashirikiana wote.
Haki ambazo wanashirikiana baina yao. Ya kwanza Kule kuwa halali maisha yao ya kindoa, na uhalali huu wanashirikiana baina yao. Yanakuwa halali ya mume kwa mkewe ambayo si halali kwa yeyote. Na hii ni haki ya wanandoa, na watakiwa kushirikiana wote kwa kuwa mmoja tu hawezi kumfaidikisha mwengine bila ya mwenzake. Ya pili ni kuharamishwa "muswaaharah", yaani mke wake anaharamika kwa mahram wote wa mume kama jinsi ni haramu kwa mama yake, mabanati zake na mahram wake wengine wote.
Tano ni kuishi kwa wema, ni wajibu kwa kila mmoja kuishi na mwenziwe kwa wema ili waishi kwa upendo na mahaba. Anasema Allaah (Jalla wa ´Alaa) katika Kitabu Chake Kitufukufu.
وَعَاشِرُوھُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.” (04:19)
وَلَھُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْھِنَّ بِالْمَعْرُوفِ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْھِنَّ دَرَجَةٌ
“Nao wanawake wanayo haki kwa Shari´aa kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.” (02:228)
Jambo la sita wawe na uaminifu kwa kila mmoja kwa mwenziwe, iwe kila mmoja anamuamini mwenziwe. Na wala asimuwekee mmoja mwenziwe shaka katika ukweli wake, nusra yake na ikhaasw yake. Na hilo kutokana na Kauli Yake Allaah (Ta´ala):
إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ
“Hakika Waumini ni ndugu.” (49:10)
Na kwa kauli ya Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
"Hatoamini mmoja wenu mpaka ampendee ndugu yake anachojipendea mwenyewe."
Ama haki za mume juu ya mke wake, kwanza ni kumtii kwa yasiyokuwa
maasi kwa Allaah na Mtume Wake. Amtii mume kwa kutimiza faradhi za dini
na kumtii Allaah (´Azza wa Jalla).Kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiya
Allaahu ´anhu) anasema kasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
“Atakaposwali mwanamke Swalah zake tano; na akafunga mwezi wake [Ramadhaan]; na akahifadhi sehemu zake za siri; na akamtii mume wake; ataingia katika mlango wowote autakao katika milango ya Jannah.”
Na kutoka kwa ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf (radhiya Allaahu ´anhu) anasema,
kasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
“Atakaposwali mwanamke Swalah zake tano; na akafunga mwezi wake [Ramadhaan]; na akahifadhi sehemu zake za siri; na akamtii mume wake; ataambiwa [Siku ya Qiyaamah]: Ingia Jannah kupitia mlango wowote uutakao katika milango ya Jannah.”
Kapokea Tirmidhiy kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiya Allaahu
´anhu)anasema, kasema Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
"Lau ningeweza kumuamrisha yeyote kumsujudia mwenziwe, ningelimua- mrisha mwanamke kumsujudia mume wake."
Kapokea Tirmidhiy kutoka kwa Ummu Salamah (radhiya Allaahu ´anha)
anasema, kasema Mtume wa Allaah ( :( صلى لله عليه وسلم
"Mwanamke yeyote akifa na mume wake yuko radhi naye, ataingia Peponi."
Angalia ewe dada wa Kiislamu, wewe uko wapi na mume wako?! Hakika yeye [ima] ndio Pepo yako au Moto wako.
Na kutoka kwa Husayn bin Muhsin kuwa ami yake alimwendea Mtume ( صلى
لله عليه وسلم ) kunako haja yake, akamaliza haja yake. Mtume ( ( صلى لله عليه وسلم
akamuuliza, je wewe una mume? Akasema "ndiyo". Akamwambia "Uko vipi
naye?" Akasema "Namfanyia kila kitu ila tu yale nisiyo yaweza."
Akamwambia [Mtume] "Angalia uko naye vipi, kwani hakika yeye [mumeo]
ndiyo Pepo yako na Moto wako."
Na katika haki kubwa ambayo ni wajibu kwa mke, ni yeye kumtii mume wake katika wakati wowote aupendao na autakao. Haki ya mume kitandani. Akimkatalia mume wake bila ya sababu ya Kishari´ah basi kafanya dhambi kubwa katika madhambi makubwa. Lakini iwe kwa sababu ya Kishari´ah. Kama mume kumwita mke wake kitandani [wafanye jimai] naye yuko na hedhi akamwambia [mke] "hapana!". Kwa kuwa haya ni maasi.
"Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba."
Ama mume wake akimuhitajia bila ya kufanya naye jimai kwenye tupu,
hakuna ubaya wala neno kama alivyokuwa akifanya Mtume wa Allaah ( صلى
لله عليه وسلم ) na wake zake. Mke akimkatalia mume wake kwa sababu moja au
nyingine kama kumletea mume akihitajiacho na kutaka, atakuwa ni mwenye
kumuasi Allaah (´Azza wa Jalla). Amefanya dhambi kubwa katika madhambi
makubwa. Sikiliza kauli ya Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) kasema:
"Naapa kwa Yule ambaye nafsi Yangu iko Mkononi Mwake, hakuna mwanaume amwitae mke wake kitandani akamkatalia isipokuwa yule Aliyeko mbinguni humkasirikia [mke] mpaka atapomridhia [mume]."
Mola (´Azza wa Jalla) Humkasirikia mpaka pale mume wake
atapomridhia.Na kutoka kwa Abu Hurayrah (radhiya Allaahu ´anhu)
anasema, kasema Mtume wa Allaah ( :( صلى لله عليه وسلم
“Mume atakapomwita mkewe kwenye kitanda chake [kwa tendo la ndoa] na yule mke akakataa kumuitika, akamkasirikia mume, Malaika humlaani mpaka kupambazuke.”
Allaahu musta´aan. Je, mwanamke kweli muumini mwenye heshima zake anaweza kuwa radhi kwa hilo?! Na ni ukubwa ulioje wanaolaaniwa kutokana na hali zao?! Allaah Atulinde.
Katika haki za mume juu ya mke wake, ni kumheshimu na kumlindia hadhi yake na kumchungia mali yake na watoto wake na kazi zilizobaki za nyumbani. Kutokana na Kauli Yake Allaah (Ta´ala):
فَالصَّالِحَاتُ قَانِتَاتٌ حَافِظَاتٌ لِّلْغَيْبِ بِمَا حَفِظَ للهُّ
“Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na wanaojilinda hata katika siri kwa kuwa Allaah Ameamrisha wajilinde.” (04:34)
Na kauli ya Mtume ( :( صلى لله عليه وسلم
"Na mwanamke ni mchungaji wa nyumba ya mume wake na watoto wake."
Na katika haki za mume juu ya mke wake, ni tabia yake [mke] nzuri na adabu
zake. Asimuudhi kwa ulimi wake wala kwa neno baya, na ajiweke mbali na
kila kitachomuondolea hadhi na haya yake. Nisikilize vizuri ewe dada wa
Kiislamu kauli ya Mtume ( صلى لله عليه وسلم ) kama ilivyo katika Hadiyth
swahiyh iliopokelewa na Tirmidhiy na ibn Hibbaan katika Hadiyth ya Abu
Darda (radhiya Allaahu ´anhu)anasema, kuwa Mtume ( ( صلى لله عليه وسلم
kasema:
"Hakuna kitu chenye uzito kwenye mizani ya muumini siku ya Qiyaamah kama tabia njema."
Nnatumai asijekudhani yeyote kuwa maneno haya ni kwa mke tu, bali hata mume pia.
Katika Hadiyth swahiyh iliopokelewa na Ahmad na ibn Hibbaan na Bazzar,
katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (radhiya Allaahu ´anhu) anasema, aliulizwa
Mtume wa Allaah ( :( صلى لله عليه وسلم
"Kitu gani kitachowafanya wengi kuingia Peponi, akasema ni "taqwa Allaah" [kumcha Allaah] na tabia njema."Na ni kipi kitachowafanya wengi kuingia Motoni? Akasema "Ni mdomo na tupu."
Ndimi na tupu, ni juu ya mke kuhifadhi sauti yake na kuzuia mikono yake kutokana na maovu, pia kwa watoto wake au ndugu zake.
Na katika haki za mume juu ya mke wake, ni kushikama [kubaki] kwenye nyumba ya mume wake. Asitoke ila kwa idhini yake na ridha yake na kuchunga jicho lake atapotoka na asitoke kwa kujishauwa. Anasema Allaah (Ta´ala):
وَقَرْنَ فِي بُيُوتِكُنَّ وَلَا تَبَرَّجْنَ تَبَرُّجَ الْجَاھِلِيَّةِ الْأُولَى
“Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani.” (33:33)
Na Anasema Allaah (Ta´ala):
وَقُل لِّلْمُؤْمِنَاتِ يَغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِھِنَّ وَيَحْفَظْنَ فُرُوجَھُنَّ وَلَا يُبْدِينَ زِينَتَھُنَّ إِلَّا مَا ظَھَرَ مِنْھَا
Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unaodhihirika. (24:31)
Na katika haki za mume juu ya mke wake, ajitengeneze na kujipamba. Katika haki kubwa ni kumuona mume mke wake akiwa mzuri.
Na mimi namnasihi kila mke kutokana na harufu mbaya sawa ya mwili au nguo. Katika mambo yanayo udhi ni kumuonamwanamke kabla ya kutoka nyumba kwenda sehemu mbali mbali za kijinga anajipamba na kujipendezesha, anabaki huko masaa na masaa ili watu wamuone ni mzuri. Anajipamba na kujipendezesha kisha anatoka barabarani. Kisha mume anapokuja kukaa naye na nguo alizoshinda nazo zenye harufu mbaya. Mume kutokana na fitrah yake, hukimbia kutokana na harufu mbaya.
Na hili linamuhusu mume pia, hata mume pia anatakiwa kujipamba na kujipendezesha kwa ajili ya mke wake. Anasema ibn ´Abbaas (radhiya Allaahu ´anhuma):
"Mimi napenda kumpambia mke wangu kama [yeye] anavyopenda kunipambia mimi."
Mwanaume pia ajipambe kwa mke wake, anukie harufu nzuri kama alivyosema ibn´Abbaas (radhiya Allaahu ´anhuma):
"Mimi napenda kumpambia mke wangu kama [yeye] anavyopenda kunipambia mimi."
Na imekuja katika Hadiyth swahiyh kutoka kwa Mtume ( ( صلى لله عليه وسلم
kasema:
"Hakika Allaah ni Jamiyl [Mzuri] na Anapenda vizuri."
Allaah ni Mzuri na Anapenda vizuri. Tahadhari kujipamba kwa mapambo ya haramu; kama kuchonga meno, kuunganisha nywele na mfano wa hayo. Haijuzu kwake mwanamke kuunganisha nywele zake kwa nywele zingine na hili ni haramu.
Na katika mapambo haramu pia ni mwanamke [wa Kiislamu] kujifananisha na mwanamke wa kikafiri katikamapambo yao na kufuata kipotofu. Hali kadhalika rangi ya kucha, na hili linazuia ufikaji wa maji. Akijipaka nayo mwanamke na akatawadha kisha akaswali wudhuu wake na swalah yake ni batili kwa kuwa maji hayakuufikia mwili.

No comments:

Post a Comment