Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, December 21, 2013

KAMPALA YAPITISHA MSWADA WA KUPINGA NDOA ZA JINSI MOJA



kampala

bunge la uganda limepitisha muswada wa sheria wa kupambana na ndoa za watu wa jinsia moja, ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo mhalifu atakayepatikana na hatia atahukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

muswada huo wa ndoa za watu jinsia moja ulipitishwa na wabunge hapo jana. taarifa zinasema kuwa, wananchi wa uganda wanamsubiri rais yoweri museveni wa nchi hiyo aidhinishe muswada huo wa bunge na kuwa sheria.

muswada huo pia unaeleza kuwa, mtu yeyote aliyekuwa na taarifa za watu wanaoshiriki ngono za watu wa jinsia moja na kushindwa kutoa taarifa hizo kwenye vyombo husika atafungwa jela maisha.

mjadala wa kuchukuliwa adhabu kali watu wanaojihusisha na ngono za jinsia moja, uliibuliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2009, lakini madola ya magharibi yaliishinikiza sana uganda, ikalazimisha kusitisha kufuatilia muswada huo.

madola ya magharibi yalitishia kusimamisha misaada yao kwa uganda kama muswada huo ungelipitishwa bungeni.

wabunge walipendekeza itumike adhabu ya kifo kwa mtu yeyote atakayepatikana kwa mara ya pili na hatia ya kujihusisha na ngono za watu wa jinsia moja au kumuambukiza mwenza wake kwa makusudi virusi vya hiv.

No comments:

Post a Comment