Serikali ya Ufaransa imeeleza azma ya kushiriki nchi hiyo kwenye
uundwaji wa kikosi cha kijeshi cha Kiafrika cha kutoa radiamali haraka
ifikapo mwaka 2015. Hayo yameelezwa na Laurent Fabius Waziri wa Mamb ya
Nchi za Nje na Jean Yves Le Drian Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa pambizoni
mwa kikao cha siku mbili cha kujadili amani na usalama barani Afrika,
kinachohudhuriwa na wakuu wa nchi za Kiafrika. Wakuu wengi wa Kiafrika
waliohutubia kikao hicho hapo jana wamesema kuwa, hivi sasa Waafrika
hawana uwezo wa kulinda amani na usalama wa bara hilo. Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje wa Ufaransa amesema kuwa, wakuu wa nchi za Kiafrika kwa
kauli moja wameafikiana suala la kupambana na makundi ya kigaidi na
maharamia katika Ghuba ya Guinea. Naye Waziri wa Ulinzi wa Ufaransa
amesema kuwa, kuna udharura wa kuundwa kikosi cha kutoa radiamali haraka
barani Afrika kitakachokuwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Afrika na
kusisitiza kuwa, Paris inaunga mkono kikamilifu suala hilo. Jean Yves Le
Drian amesema kuwa suala la maharamia katika Ghuba ya Guinea
litajadiliwa kwenye Baraza la Ulaya hivi karibuni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment