Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, December 7, 2013

Bandar bin Sultan aendeleza njama dhidi ya Syria


Bandar bin Sultan aendeleza njama dhidi ya Syria
Bandar bin Sultan bin AbdulAziz Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Saudi Arabia ameelekea nchini Russia kwa shabaha ya kupanga mikakati mipya dhidi ya serikali ya Syria. Taarifa zinasema kuwa, safari ya Bandar bin Sultan ina lengo la kufanya njama za kukwamisha kikao cha Geneva 2 na kuimarisha nguvu za wapinzani na makundi ya kigaidi yanayopambana na serikali ya Syria. Itakumbukwa kuwa, Mwanamfalme huyo wa Saudi Arabia alionyesha radiamali kali baada ya kufikiwa makubaliano ya awali ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5 + 1 mjini Geneva hivi karibuni. Hii ni mara ya pili kwa Bandar bin Sultan kufanya safari nchini Russia katika kipindi cha miezi minne iliyopita. Katika safari iliyopita, alitoa pendekezo kwa viongozi wa Russia la kuitaka nchi hiyo iache kuiunga mkono Syria, mkabala wa Saudi Arabia kununua silaha na zana za kijeshi zenye thamani ya dola bilioni 15, pendekezo ambalo lilipingwa vikali na viongozi wa Moscow. Saudi Arabia inawapatia misaada ya kifedha na kisilaha makundi ya Geneva
Kisalafi na yale yanayowakufurisha Waislamu wengine, kwa lengo la kushadidisha machafuko nchini Syria, na hatimaye kuangushwa utawala wa Rais Bashar Assad wa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment