Askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa waliko mashariki mwa nchi hiyo wamepeleka misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja na chakula kwa waasi wa zamani wa Kongo wa kundi la M23 wanaohifadhiwa katika eneo lililoko umbali wa kilomita 40 kutoka mji wa Goma katika mkoa wa Kivu Kaskazini. Jenerali Tim Mukunto wa jeshi la Kongo amesema karibu tani 10 za chakula zinazotosha kwa ajili ya kipindi cha wiki mbili zimekabidhiwa kwa waasi hao wa zamani.
Awali askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na taasisi mbalimbali za kimataifa zilielezea wasiwasi wao kuhusu hali mbaya ya waasi wa zamani wa kundi la M23 nchini Kongo.
Kundi hilo la waasi wa zamani lililazimika kutia saini makubaliano ya amani na serikali ya Kinshasa baada ya kupata kipigo kikubwa katika operesheni ya kijeshi iliyoshirikisha jeshi la Kongo na askari wa kimaraifa.
No comments:
Post a Comment