skip to main |
skip to sidebar
Wahajiri wa Kiafrika wafungwa jela bila mashtaka Israel
Utawala wa Kizayuni wa Israel umewafunga jela wahajiri 480 wa
Kiafrika, na idadi hiyo inaweza kuongezeka hadi kufikia 1,000 mwishoni
mwa mwaka huu. Kwa mujibu wa sheria iliyopitishwa na Bunge la Israel
wiki iliyopita, viongozi wa Israel wanaweza kuwaweka korokoroni wahajiri
wa Kiafrika kwa muda wa mwaka mmoja bila ya kuwafungulia mashtaka. Hivi
karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel ulipitisha mpango mpya ulio
dhidi ya wahajiri elfu hamsini wa Kiafrika, ambao unatoa adhabu kali
dhidi ya Waafrika wanaofanya kazi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Wakati huohuo, Taasisi ya Wahajiri ya Israel imeeleza kuwa, tokea
kuanza mwaka huu wa 2013 zaidi ya wahajiri 1,600 kutoka Eritrea na Sudan
wamefukuzwa huko Israel na kurejeshwa makwao. Hayo yanajiri katika hali
ambayo, wahajiri wa Kiafrika wameshafanya maandamano mara kadhaa
wakilalamikia vitendo hivyo vya kibaguzi na unyanyasaji, ingawa
waandamanaji hao wamekuwa wakishambuliwa kwa mabomu ya machozi na risasi
za plastiki na vikosi vya usalama vya Israel.
No comments:
Post a Comment