Maafisa nchini Misri wamemuondolea Ahmad Shafiq marufuku ya 
kusafiri nje ya nchi. Shafiq alikuwa waziri mkuu wa mwisho wa Hosni 
Mubarak dikteta aliyeng’olewa madarakani katika mapinduzi ya wananchi 
huko Misri.  Mamlaka inayohusika na hati za kusafiria ya Misri 
imewaagiza maafisa wa uwanja wa ndege kuliondoa jina la Jenerali Ahmad 
Shafiq katika orodha ya watu wasioruhusiwa kusafiri nje baada ya 
kutopatikana na hatia katika kesi ya ardhi ya marubani.
Hayo yemeelezwa na duru moja ya kiwanjani hapo ambayo haikutaja jina lake. Kuondolewa kwa marufuku hiyo ya kusafiri kumejiri baada ya mahakama moja ya Misri kuwafutia mashtaka ya ubadhirifu tarehe 19 mwezi huu, waziri mkuu huyo wa zamani na pia watoto wawili wa dikteta Hosni Mubarak yaani Alaa na Gamal.
Ahmad Shafiq alikuwa anakabiliwa na mashtakiwa ya kuwauzia ardhi ya serikali kinyume cha sheria watoto hao wawili wa dikteta Mubarak tena kwa bei ya chini kabisa.
   
No comments:
Post a Comment